Mwamnyeto akiri Bocco ndio mwenyewe

BEKI wa Coastal Union, Bakar Mwamnyeto amekiri kwamba anapendezewa na aina ya uchezaji wa John Bocco wa Simba, akisema ana kila kitu cha kuwa mshambuliaji kama walivyo mastaa wkubwa wa Ulaya.

Alimchambua Bocco akisema ana uwezo wa kukaa na mpira, anajua kukaa nafasi yake, anajua kufunga na anatoa pasi kwa uharaka anapoona beki.

Alisema tangu aanze kucheza mpira ndiye straika anayemkubali na kumvutia uchezaji wake na kukiri anasumbua mabeki.

“Bila wivu wala kupepesa macho, Bocco anafiti kwenye nafasi yake, bila shaka wanaocheza nafasi yake wanatamani kuwa kama yeye, pia bodi yake ni ya mpira,”

“Bocco ni mrefu anaweza akafunga mabao ya kichwa na miguu, hilo ndio mwiba kwa mabeki kumsoma kwa haraka kujua anaweza akaleta madhara gani,” alisema.

Mwanyeto, ambaye hivi karibuni alikuwa anahusishwa na kutakiwa na Simba na Yanga, alisema  anaamini uwezo wa Bocco ni msaada katika timu ya Taifa Stars.