Mshambuliaji Nchimbi wa Azam asaini Polisi Tanzania

Monday July 15 2019

Mwanaspoti, Mshambuliaji Nchimbi, wa Azam asaini, Polisi Tanzania, Mwanasport, Michezo

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Azam, Ditram Nchimbi amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Ditram alisajiliwa Azam msimu uliopita akitokea Njombe Mji lakini hakupata nafasi ya kuichezea katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Kombe la Kagame.

Hali hiyo ilimlazimu kutoka kwa mkopo msimu uliopita na kujiunga na Mwadui katika dirisha dogo alikuwa akiichezea na aliweza kutengeneza kombinesheni nzuri akiwa na mshambuliaji mwenzake Salim Aiyee ambaye amejiunga na KMC.

Akiwa katika kikosi cha Mwadui alifunga magoli matano na kutoa pasi za magoli 13 katika msimu uliopita.

Mshambuliaji huyu alishindwa kusafili na wachezaji wenzake kuelekea nchini Rwanda katika mashindano ya Kagame Cup baada ya kocha Ettienne Ndayiragije kutokuwa katika mipango ya kocha huyo.

Advertisement