Kenya v Senegal: Takwimu zinaonesha Harambee Stars haina ubavu kwa Simba wa Teranga

Monday July 1 2019

Kenya v Senegal, Takwimu zinaonesha, Harambee Stars haina ubavu, kwa Simba wa Teranga, Mwanasport, Mwanaspoti, Michezo

 

By Fadhili Athumani

Cairo, Misri. Utakuwa ni Mchezo wa kufa ua kupona pale uwanja wa Jeshi, maarufu kama 30 June Cairo Stadium, utakapokuwa mwenyeji wa mashabiki 30,000 watakaofurika uwanjani kushuhudia mechi ya mwisho wa Kundi C, kati ya Kenya dhidi ya Senegal.

Mechi hii, itakayochezwa majira ya saa nne usiku, sambamba na ile ya Tanzania Vs Algeria, utaamua ni nani ataungana na Alegeria katika hatua ya 16 bora, kutokea kundi C. Huku wakenya wakiwa na matumaini ta kushuhudia Samsoni akimuua Simba wakali kutoka milima ya Teranga, takwimu kati ya timu hizi mbili inasema vinginevyo.

Kenya, iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi C, ilijiongezea matumaini ya kuvuka hatua haya ya makundi, baada ya kuwatandika majirani zao Tanzania 3-2, huku Senegal, inayoshika nafasi ya pili, ikijiweka katika wakati mgumu baada ya kuchapwa na Algeria 1-0. Zinaingia kwenye mchezo wa leo, zikihitaji ushindi. Itakuaje?

Rekodi inaonesha kuwa, Kenya inayoshiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15, haijawahi kufunga bao hata moja dhidi ya Senegal, ambao wanawinda taji lao la kwanza. Mara ya mwisho kwa pande hizi mbili kukutana ilikuwa ni mwaka 2004, katika fainali zilizofanyika huko Tunisia, kwenye hatua kama hii, ambapo Stars ilitandikwa 3-0.

Timu hizi mbili zimekutana mara tatu huko nyuma, ambapo katika mechi hizo tatu, Kenya imeambulia sare tasa mara moja, huku ikifungwa mara mbili. Leo wanakutana kwa mara ya nne. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa, katika mechi tatu za tatu za Afcon, Kenya imeshinda michezo miwili, huku Senegal wao, wakipoteza mara moja tu, katika mechi zao sita za Afcon.

Stars, inayonolewa na Sebastien Migne, watakuwa na kazi kubwa ya kuimarisha safu yao ya ulinzi, hasa wanapokutana na safu hatari ya ushambuliaji inayoongozwa na Sadio Mane, kwani mahesabu yanaonesha kuwa katika michezo yake nane ya hivi karibuni, beki ya Kenya imeruhusu mabao 17. Mshindi atafuzu moja kwa moja, huku atakayefungwa atajiweka katika nafasi nafasi ya kufuzu kama 'best looser'.

Advertisement

Advertisement