Majeraha yamuondoa Nyoni Stars

Saturday November 16 2019

 

By Thomas Ng'itu

TAIFA Stars imeoendoka alfajiri ya leo Jumamosi kuwafuata Libya ikiwa ni mechi yao ya pili Kundi J kuwani kufuzu fainali za Afcon huku ikimuacha beki wao Erasto Nyoni.
Stars itacheza na Libya wiki ijayo, Novemba 19 ambapo Nyoni ameshindwa kuwa miongoni mwa nyota walioondoka baada ya kupata majeraha ya goti.
Immelezwa kwamba mchezaji huyo alipata majeraha hayo katika mechi dhidi ya Guinea ya Ikweta ambapo Stars ilishinda bao 2-1 jana Ijumaa uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Nyoni alicheza dakika zote 90 huku dakika 45 za kipindi cha kwanza alicheza kiungo mkabaji na dakika 45 za kipindi cha pili alicheza beki wa kati.
Kukosekana kwa Nyoni kutamfanya Bakari Mwamnyeto kucheza na Kelvin Yondani kama ilivyokuwa jana.
Mwamnyeto aliendelea kuonyesha utulivu ambao alianza nao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda pamoja na ule wa Sudan mechi ya kufuzu fainali za CHAN.

Advertisement