Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zimeanza kwa kutoa dozi mfululizo Ligi Kuu England

LONDON, ENGLAND. LIVERPOOL, Arsenal na Manchester United zimeshawahi kuwa na rekodi ya kushinda mechi mfululizo kwenye Ligi Kuu England, lakini bado haikutajwa kuwa mwenendo bora zaidi.

Manchester City imekuwa ikifanya hivyo kwa kuwa na mwanzo mzuri wa kushinda mechi mfululizo kwa misimu kadhaa kwenye Ligi Kuu England. Rekodi zinaonyesha kuna timu sita tu zilizowahi kushinda mfululizo mara nyingi zaidi kwenye mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu England.

Na sasa Man City ya Pep Guardiola itahitaji kushinda dhidi ya Nottingham Forest (nyumbani), Wolves (ugenini), Arsenal (ugenini), Brighton (nyumbani) na Man United (ugenini) kuandika rekodi mpya. Kila la heri.

Cheki hapa mwanzo mzuri wa kushinda mechi mfululizo kwenye Ligi Kuu England.


Aston Villa (2020/21, mechi 4)

Imezifunga: Sheffield United (1-0), Fulham (0-3), Liverpool (7-2), Leicester (0-1)

Iliyotibua rekodi: Leeds United (3-0, uwanjani Villa Park).

Walivyomaliza  msimu: Aston Villa ilimaliza msimu huo ikiwa kwenye nafasi ya 11.


 Everton (2020/21, mechi 4)

Imezifunga: Tottenham (0-1), West Brom (5-2), Crystal Palace (1-2), Brighton (4-2)

Iliyotibua rekodi: Liverpool (2-2, uwanjani Goodison Park).

Ilivyomaliza msimu: Everton ilimaliza msimu huo kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu England.


Watford (2018/19, mechi 4)

Imezifunga: Brighton (2-0), Burnley (1-3), Crystal Palace (2-1), Tottenham (2-1)

Iliyotibua rekodi: Man United (2-1, uwanjani Vicarage Road).

Ilivyomaliza msimu: Katika msimu huo iliyoanza vizuri kabisa, Watford ilishika nafasi ya 11 katika siku ya mwisho ya msimu na Javi Gracia alikabidhiwa mkataba mpya.

 

Chelsea (2014/15, mechi 4)

Imezifunga: Burnley (1-3), Leicester (2-0), Everton (3-6), Swansea (4-2)

Iliyotibua rekodi: Man City (1-1, uwanjani Etihad)

Ilivyomaliza msimu: Chelsea, katika msimu huo ilioanza kibabe kabisa ilifanikiwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England, huku mechi yake ya kwanza ya msimu iliichapa Burnley ugenini huku benchi lake alikuwa Jose Mourinho.


-Man City (2011/12,mechi 4)

Imezifunga: Swansea (4-0), Bolton (2-3), Tottenham (1-5), Wigan (3-0)

Iliyotibua rekodi: Fulham (2-2, uwanjani Craven Cottage).

Walivyomaliza msimu: Man City ilimaliza msimu huo wakiwa mabingwa, huku straika wao Edin Dzeko alifunga mara sita na Sergio Aguero alifunga mara nne katika mechi nne za kwanza kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huo.


Tottenham (2009/10, mechi 4)

Imezifunga: Liverpool (2-1), Hull (1-5), West Ham (1-2), Birmingham (2-1)

Iliyotibua rekodi: Man United (3-1, uwanjani Old Trafford).

Walivyomaliza msimu: Top Four. Spurs ilimaliza msimu huo ikiwa nafasi ya nne na hivyo kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa chini ya kocha Harry Redknapp.


Man United (2006/07, mechi 4)

Imezifunga: Fulham (5-1), Charlton (3-0), Watford (2-1), Tottenham (1-0)

Iliyotibua rekodi: Arsenal (1-0, uwanjani Old Trafford).

Walivyomaliza msimu: Kwa msimu huo, Man United ilifanikiwa kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England, pointi sita zaidi ya timu iliyoshika namba mbili, ambao walikuwa Chelsea.


Charlton (2005/06, mechi 4)

Imezifunga: Sunderland (1-3), Wigan (1-0), Middlesbrough (0-3), Birmingham (0-1)

Iliyotibua rekodi: Chelsea (2-0, uwanjani The Valley).

Walivyomaliza msimu: Charlton ilimaliza nafasi ya 13, huku asilimia 30 ya ushindi wa mechi zao kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huo ilikuwa kwenye mechi zao nne za mwanzo.


Chelsea (2004/05, mechi 4)

Imezifunga: Man United (1-0), Birmingham (0-1), Crystal Palace (0-2), Southampton (2-1)

Iliyotibua rekodi: Aston Villa (0-0, uwanjani Villa Park).

Walivyomaliza msimu: Katika msimu huo, Chelsea ilibeba ubingwa wa Ligi Kuu England na huo ulikuwa mwanzo wa kocha Jose Mourinho kubeba taji hilo, ambapo timu yake ilipoteza mechi moja tu na kuruhusu mabao 15 pekee katika mechi 38.


Arsenal (2003/04, mechi 4)

Imezifunga: Everton (2-1), Middlesbrough (0-4), Aston Villa (2-0), Man City (1-2)

Iliyotibua rekodi: Portsmouth (1-1, uwanjani Highbury).

Ilivyomaliza msimu: Msimu huo, Arsenal ilicheza bila ya kupoteza mchezo hata mmoja na kufanikiwa kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.


Sheffield Wednesday (1996/97, mechi 4)

Imezifunga: Aston Villa (2-1), Leeds (2-0), Newcastle (2-1), Leicester (2-1)

Iliyotibua rekodi: Chelsea (2-0 uwanjani Stamford Bridge).

Ilivyomaliza msimu: Nafasi ya saba. Sheffield Wednesday maarufu kama “The Owls” ilianza msimu huo kwa kishindo kama bomu chini ya kocha wake David Pleat.


Newcastle (1995/96, mechi 4)

Imezifunga: Coventry (3-0), Bolton (1-3), Sheffield Wednesday (0-2), Middlesbrough (1-0)

Iliyotibua rekodi: Southampton (1-0 uwanjani The Dell).

Ilivyomaliza msimu: Newcastle United kwenye msimu huo ilishindwa kidogo tu kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England, ambapo ilimaliza kwenye nafasi ya pili.


Arsenal (2022/23, mechi 5)

Imezifunga: Crystal Palace (0-2), Leicester (4-2), Bournemouth (0-3), Fulham (2-1), Aston Villa (2-1)

Iliyotibua rekodi: Man United (3-1 uwanjani Old Trafford).

Ilivyomaliza msimu: Hiyo ilikuwa msimu uliopita, ambapo Arsenal ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi licha ya kuongoza kwa muda mrefu, ikashindwa kuchukua ubingwa.


 Chelsea (2018/19, mechi 5)

Imezifunga: Huddersfield (0-3), Arsenal (3-2), Newcastle (1-2), Bournemouth (2-0), Cardiff (4-1)

Iliyotibua rekodi: West Ham United (0-0 uwanjani London).

Ilivyomaliza msimu: Nafasi ya tatu. Kwenye benchi lake la ufundi kocha alikuwa Maurizio Sarri, lakini baadaye ikaachana naye na kumleta Frank Lampard.


 Man City (2015/16, mechi 5)

Imezifunga: West Brom (0-3), Chelsea (3-0), Everton (0-2), Watford (2-0), Crystal Palace (0-1)

Iliyotibua rekodi: West Ham (2-1 uwanjani Etihad).

Ilivyomaliza msimu: Namba nne. Ushindi kwenye mechi tano huku ikiwa haijaruhusu bao lolote kwenye mechi hizo ulikuwa mwanzo mzuri wa Man City kwenye Ligi Kuu England msimu huo, ambapo Pep Guardiola ndiyo kwanza alikuwa amewasili.


Man United (2011/12, mechi 5)

Imezifunga: West Brom (1-2), Tottenham (3-0), Arsenal (8-2), Bolton (0-5), Chelsea (3-1)

Iliyotibua rekodi: Stoke City (1-1 uwanjani Britannia)

Ilivyomaliza msimu: Nafasi ya pili, ikiwakaribia kabisa ubingwa kwenye Ligi Kuu England msimu huo, ambao ilikuwa Manchester City.


Chelsea (2010/11, mechi 5)

Imezifunga: West Brom (6-0), Wigan (0-6), Stoke (2-0), West Ham (1-3), Blackpool (4-0)

Iliyotibua rekodi: Man City (1-0 uwanjani Etihad).

Ilivyomaliza msimu: Katika msimu huo, Chelsea ilimaliza Ligi Kuu England katika nafasi ya pili kwenye msimamo na hiyo ilionekana nafasi mbaya na Carlo Ancelotti akafutwa kazi.


Arsenal (2004/05, mechi 5)

Imezifunga: Everton (1-4), Middlesbrough (5-3), Blackburn (3-0), Norwich (1-4), Fulham (0-3)

Iliyotibua rekodi: Bolton (2-2 uwanjani Highbury).

Ilivyomaliza msimu: Nafasi ya pili. Staa Jose Antonio Reyes alifunga katika kila mechi kwenye zile tano za mwanzo kwa msimu huo, lakini Chelsea ndio iliyomaliza ikiwa kileleni.


Liverpool (2018/19, mechi 6)

Imezifunga: West Ham (4-0), Crystal Palace (0-2), Brighton (1-0), Leicester (1-2), Tottenham (1-2), Southampton (3-0)

Iliyotibua rekodi: Chelsea (1-1 uwanjani Stamford Bridge).

Ilivyomaliza msimu: Nafasi ya pili. Nafasi ya pili bora zaidi kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England, huku Liverpool ilibeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huo.


Man City (2016/17, mechi 6)

Imezifunga: Sunderland (2-1), Stoke (1-4), West Ham (3-1), Man United (1-2), Bournemouth (4-0), Swansea (1-3)

Iliyotibua rekodi: Tottenham (2-0 uwanjani White Hart Lane).

Ilivyomaliza msimu: Namba tatu. Kocha Pep Guardiola alifikia rekodi ya Carlo Ancelotti kwenye Ligi Kuu England kwa kushinda mfululizo kwenye mechi sita za mwanzo kwenye ligi hiyo.


Chelsea (2009/10, mechi 6)

Imezifunga: Hull (2-1), Sunderland (1-3), Fulham (0-2), Burnley (3-0), Stoke (1-2), Tottenham (3-0)

Iliyotibua rekodi: Wigan (3-1 uwanjani DW).

Ilivyomaliza msimu: The Blues ilimaliza msimu huo ikinyakua taji la Ligi Kuu England sambamba na Kombe la FA. Hakika haukuwa msimu mbaya kwa upande wake.


Newcastle (1994/95, mechi 6)

Imezifunga: Leicester (1-3), Coventry (4-0), Southampton (5-1), West Ham (1-3), Chelsea (4-2), Arsenal (2-3)

Iliyotibua rekodi: Liverpool (1-1 uwanjani St James’ Park).

Ilivyomaliza msimu: Namba sita. Baada ya kuanza kibabe kabisa kwenye ligi kwa msimu huo, Newcastle ilionyesha kuna kitu inahitaji kukifanya ndani ya uwanja na kuvutia wengi.


Liverpool (2019/20, mechi 8)

Imezifunga: Norwich (4-1), Southampton (2-1), Arsenal (3-1), Burnley (3-0), Newcastle (3-1), Chelsea (2-1), Sheffield United (1-0), Leicester (2-1)

Iliyotibua rekodi: Man United (1-1 uwanjani Old Trafford).

Ilivyomaliza msimu: Katika msimu huo, ambao Liverpool ilianza kwa kushinda mechi nane mfululizo kwenye Ligi Kuu England ilifanikiwa kunyakua ubingwa.


Chelsea (2005/06, mechi 9)

Imezifunga: Wigan (0-1), Arsenal (1-0), West Brom (4-0), Tottenham (0-2), Sunderland (2-0), Charlton (0-2), Aston Villa (2-1), Liverpool (1-4), Bolton (5-1)

Iliyotibua rekodi: Everton (1-1 uwanjani Goodison Park).

Ilivyomaliza msimu: Mabingwa. Msimu huo, Chelsea ilikuwa ngumu kwelikweli kuruhusu bao hadi hapo, Luke Moore alipoweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga dhidi ya Chelsea baada ya dakika 641 kwenye Ligi Kuu England.