Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yorke: Palmer? Ni Liverpool tu

Yorke Pict (1)
Yorke Pict (1)

Muktasari:

  • Palmer, 22, amejitengeneza kama mmoja wa wachezaji vijana matata kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Manchester City kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, akichangia zaidi ya mabao 33 katika msimu wa 2023-24.

LONDON, ENGLAND: GWIJI wa Ligi Kuu England, Dwight Yorke amesema Cole Palmer atataka kuhama Chelsea endapo itashindwa kumaliza Top Four kwenye Ligi Kuu England msimu huu - lakini anachokiona ni Mwingereza huyo atatua Liverpool.

Palmer, 22, amejitengeneza kama mmoja wa wachezaji vijana matata kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Manchester City kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, akichangia zaidi ya mabao 33 katika msimu wa 2023-24.

Bahati mbaya kwa Palmer na Chelsea, mambo yamekuwa magumu msimu huu. Kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca kinapambana kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, huku Palmer akicheza mechi saba bila kufunga bao.

Na kinachoelezwa ni kiungo huyo mshambuliaji ataachana na miamba ya Stamford Bridge endapo kama itashindwa kumaliza ndani ya Top Four. Yorke haoni hilo likitokea, licha ya kwamba anadhani Palmer atachukuliwa na miamba ya Anfield kwenda kurithi mikoba ya Mohamed Salah akiondoka.

Yorke aliulizwa kuhusu uwezekano wa Palmer kuhama Chelsea, alisema: "Mimi hainingii akilini. Sidhani kama atataka kuondoka Chelsea kama itashindwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Bado kijana mdogo na alipotua kwenye timu hiyo ndiyo amefanya kiwango chake kuwa bora. Kwanini aondoke kwenye timu iliyomfanya kuwa mchezaji mzuri ndani ya siku chache?

"Wapi atakwenda kuwa mchezaji mkubwa na tegemeo? Liverpool? Labda Man United, alisema yeye ni shabiki wa Man United, lakini hawezi kwenda huko kwa sababu yeye ni mtu wa Man City. Nje ya hizo ni Arsenal, hawezi kwenda huko kwa sababu Bukayo Saka yupo.

"Liverpool inaweza kumfikiria kama Mo Salah ataondoka, hivyo ni mtu ambaye wanaweza kumfikiria. Hivyo, subirini kama Mo Salah ataondoka."

Wakati Palmer na Chelsea wakiwa kwenye nyakati ngumu, Mo Salah hatima yake kwenye klabu ya Liverpool bado haieleweki na mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na hakuna dili lolote jipya lililoafikiwa kusainiwa. Mo Salah amechangia zaidi ya mabao 50 kwenye michuano yote akiwa na kikosi cha Liverpool msimu huu.