Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe: Yoyote aje awe Ubelgiji au Hispania

MWAMBA Pict

Muktasari:

  • Mbappe aliyetangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kwa mara nyingine, amesema jambo muhimu kwa sasa ni kuendelea na safari ya kutafuta ubingwa, bila kujali kama watacheza dhidi ya Ubelgiji au Hispania.

DALLAS, MAREKANI: NAHODHA wa Ufaransa, Kylian Mbappe amesema hana upendeleo wa mpinzani watakayekutana naye katika nusu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuiongoza timu yake kuiondoa Morocco kwa ushindi wa mabao 2-0.

Mbappe aliyetangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kwa mara nyingine, amesema jambo muhimu kwa sasa ni kuendelea na safari ya kutafuta ubingwa, bila kujali kama watacheza dhidi ya Ubelgiji au Hispania.

“Haijalishi kwangu. Kama itakuwa Ubelgiji, basi tutacheza na Ubelgiji. Kama ni Hispania, basi tutacheza na Hispania. Tutasubiri tuone kitakachotokea. Hii ni nusu fainali na mechi yoyote itakuwa ngumu.”

MWAMB 03

Mbappe pia alizungumza kuhusu nafasi yake ya uongozi ndani ya kikosi cha Ufaransa, akisema sasa anajiona akiwa na jukumu kubwa zaidi, hasa nje ya uwanja.

“Ninajisikia vizuri nikiwa na timu ya taifa ya Ufaransa. Hiki ni kikosi ninachokipenda sana na wengi wa wachezaji ni marafiki zangu wa muda mrefu.”

Aliendelea: “Pia kuna vijana wadogo ambao sasa wananiona kama mmoja wa wachezaji wakubwa. Lazima niwe mfano kwao, hasa upande wa kisaikolojia na kihisia.”

MWAMB 02

Mbappe amesema uzoefu wake mkubwa katika Kombe la Dunia unampa wajibu wa kuwaongoza wenzake.

“Mambo yanayotokea uwanjani ni soka, lakini upande wa hisia nina uzoefu mkubwa kwa sababu nimecheza mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye kikosi hiki. Ni jukumu langu kuwashirikisha uzoefu huo wenzangu.”

MWAMB 06

Atoa taarifa kuhusu jeraha la kifundo cha mguu

Nahodha huyo pia alituliza hofu kuhusu jeraha lililomlazimu kutoka uwanjani mwishoni mwa mchezo dhidi ya Morocco.

“Niko sawa. Nilipata maumivu kwenye kifundo cha mguu, lakini hali yangu ni nzuri. Mateta alikuwa kwenye hali nzuri zaidi ya kucheza dakika 15 za mwisho.”

Mbappe amesema Ufaransa bado haijafikia lengo lake.

“Tunajua njia pekee ya kuwa na furaha ni kushinda. Tuko nusu fainali na tunafurahia hatua tuliyofikia, lakini bado safari ni ndefu. Tunajua yaliyopo mbele yatakuwa magumu zaidi kuliko tuliyopitia, lakini tuko tayari kukabiliana nayo.”

MWAMB 05

Azungumzia kumtoa rafiki yake Hakimi

Mbappe pia alizungumzia hisia zake baada ya kumng’oa kwenye mashindano rafiki yake mkubwa, Achraf Hakimi wa Morocco.

“Hapana, hisia zitakuja nitakapomuona tena kwenye chumba cha kubadilishia nguo, kwa sababu huko ndipo tunarudi kuwa marafiki na binadamu wa kawaida.”

Aliongeza:”Uwanjani hakuna urafiki. Kila mmoja alikuja kushinda. Yeye alitaka kushinda na mimi pia nilitaka kushinda.”

“Nitakapokutana naye tena baada ya mechi, bila shaka itanigusa kwa sababu ni rafiki yangu wa karibu sana. Lakini ndani ya uwanja hakuna nafasi ya hisia.”

“Bado hatujafikia kiwango cha mabingwa wa 2018”

Mbappe pia aliulizwa kama kikosi cha sasa cha Ufaransa ndicho bora zaidi kuwahi kucheza nacho, hata kuliko kile kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018.

MWAMB 01

Mshambuliaji huyo hakukubaliana na hoja hiyo.

“Hapana. Mimi tayari nimekuwa bingwa wa dunia na pia mshindi wa pili wa Kombe la Dunia. Kikosi hiki bado hakijawa bingwa wala mshindi wa pili.”

Hata hivyo, alikiri kuwa timu ya sasa ina vipaji vikubwa na mustakabali mzuri.

“Hiki ndicho kikosi chenye uwezo mkubwa zaidi na ambacho ni rahisi kuona kinaweza kufanya makubwa siku zijazo. Kina ubora mkubwa na kinawapa watu matumaini.”

Mbappe alihitimisha kwa kusisitiza ubora wa timu hupimwa kwa mataji, si kwa majina ya wachezaji.

“Timu bora ni ile inayobeba mataji. Kwa sasa sioni kombe la dhahabu pembeni yangu.”