Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klabu yamzuia beki Mbelgiji kucheza dhidi Hispania

KLABU Pict

Muktasari:

  • Debast, mwenye umri wa miaka 22, hajacheza hata dakika moja kwenye mashindano hayo baada ya kuumia mwishoni mwa msimu wa ligi nchini Ureno.

LOS ANGELES, MAREKANI: Beki wa Ubelgiji, Zeno Debast, amejikuta katikati ya mvutano mkubwa kati ya timu yake ya taifa na klabu yake ya Sporting Lisbon, huku akitarajiwa kuukosa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania utakaochezwa leo.

Debast, mwenye umri wa miaka 22, hajacheza hata dakika moja kwenye mashindano hayo baada ya kuumia mwishoni mwa msimu wa ligi nchini Ureno.

Baada ya kurejea mazoezini mwishoni mwa Juni, kulikuwa na matumaini kuwa angekuwa fiti kwa ajili ya hatua za mtoano, lakini mvutano wa kitabibu kati ya Shirikisho la Soka la Ubelgiji (RBFA) na Sporting umevuruga mipango hiyo.

KLAB 01

Kupitia taarifa rasmi, RBFA imesema Sporting imeiambia Debast kuwa bado hajawa tayari kiafya kucheza mechi, jambo ambalo linapingana na tathmini ya madaktari wa timu ya taifa ya Ubelgiji pamoja na madaktari wa FIFA.

"Zeno Debast hatakuwa sehemu ya mchezo wa robo fainali. Klabu yake ya Sporting CP imemjulisha kuwa bado haijamruhusu kucheza kutokana na hali yake ya afya. Tathmini hiyo inatofautiana na ile ya madaktari wa Red Devils pamoja na wataalamu wa afya na bima wa FIFA," ilisema sehemu ya taarifa ya RBFA.

Kwa sasa Debast anaendelea kufanya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa kitengo cha utendaji wa RBFA.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Sporting na RBFA zimekuwa zikiwasiliana kila siku tangu kuanza kwa Kombe la Dunia kuhusu maendeleo ya beki huyo, huku kikao maalumu kati ya pande hizo kikitarajiwa kufanyika Los Angeles kabla ya mchezo dhidi ya Hispania.

KLAB 02

Debast tayari ameichezea Ubelgiji mechi 26 za kimataifa na pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia 2022.

Katika mashindano haya ameonekana mara nyingi akifanya mazoezi peke yake huku akiendelea kuwapa sapoti wenzake kutoka pembeni ya uwanja.


UBELGIJI BADO INA IMANI

Licha ya kuukosa mchango wa Debast, Ubelgiji imeendelea kufanya vizuri katika Kombe la Dunia.

Baada ya kuongoza kundi lao kwa pointi tano, walifanya comeback ya kusisimua dhidi ya Senegal katika hatua ya 32 Bora kabla ya kuichapa Marekani mabao 4-1 kwenye hatua ya 16 Bora na kutinga robo fainali.

Kocha wa Ubelgiji, Rudi Garcia, amesema kikosi chake kinafahamu ukubwa wa kazi inayowasubiri dhidi ya Hispania, lakini hakina sababu ya kuogopa.

KLAB 03

"Tunajua tunacheza dhidi ya moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa. Hispania ni moja ya timu bora zaidi duniani katika umiliki wa mpira na wamekuwa wakicheza kwa mfumo huo kwa zaidi ya miaka 15," alisema Garcia.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa Ubelgiji ina uwezo wa kuleta ushindani mkubwa.

"Sisi pia tuna kikosi kizuri. Ni timu ya pili yenye mabao mengi kwenye mashindano haya, wakati wao wanaongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Tunaamini tunaweza kufanya kitu maalumu."

Garcia aliongeza kuwa presha ya mashabiki haitawazuia kupambana.

"Tuliiondoa Marekani kwenye uwanja ambao mashabiki wote walikuwa wanaiunga mkono. Mashabiki hawafungi mabao. Tutazingatia uwezo wetu na kufanya kila linalowezekana kuipa Hispania ushindani mkubwa."