Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wirtz amaliza utata Liverpool

Muktasari:

  • Taarifa zinadai usajili wa staa huyo ni kama umeshakamilika kwa asilimia kubwa na muda wowote Liverpool na Bayer Leverkusen zinaweza kufikia mwafaka juu ya ada ya uhamisho na staa huyo atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kupata Pauni 18.5 milioni kwa mwaka.

LEVERKUSEN, UJERUMANI: WAKATI Bayer Leverkusen ikiendelea msimamo wake wa kuhitaji zaidi ya Pauni 125 milioni ili kumuuza staa wao  Florian Wirtz  kwenda Liverpool, ripoti zinaeleza staa huyo amewaambia mabosi kuwa hataki tena kuendelea kubakia Leverkusen na lifanyike liwezekanalo atue zake Liverpool kwani ndiyo sehemu anayotaka kucheza kwa msimu ujao.

Taarifa zinadai usajili wa staa huyo ni kama umeshakamilika kwa asilimia kubwa na muda wowote Liverpool na Bayer Leverkusen zinaweza kufikia mwafaka juu ya ada ya uhamisho na staa huyo atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kupata Pauni 18.5 milioni kwa mwaka.

Leverkusen wanataka Pauni 120 milioni, huku Liverpool tayari wakiwa wamesimamia kwenye ofa ya Pauni 109 milioni. Hata hivyo, Wirtz ameeleza wazi anataka kujiunga na Liverpool.

Inatarajiwa Wirtz atakamilisha vipimo vya afya wiki ijayo kabla ya kwenda likizo na kisha kujiunga na kikosi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Julai.

Nyota huyo wa Ujerumani amevutiwa na mpango wa Kocha Arne Slot aliyemwambia atamtumia kama mchezaji wa namba 10.

Jumatano, baada ya mechi ya Uefa Nations League dhidi ya Ureno,  Wirtz alionekana kutikisa kichwa ikiwa ni ishara ya kukubali alipoulizwa na tovuti ya MailSport kama “anafurahia kujiunga na Liverpool”.

Iwapo Liverpool watakubali matakwa ya Leverkusen, Wirtz atakuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa katika historia ya soka la England.

Moja kati ya sababu zinazodaiwa kusababisha Leverkusen izidishe bei ni  kanuni za FIFA ambazo zinaeleza, timu yoyote iliyochangia maendeleo ya mchezaji kati ya umri wa miaka 12 hadi 23 inastahili asilimia tano ya ada ya uhamisho kama fidia ya mafunzo.

Timu ya FC Koln ambayo Wirtz alijiunga nayo akiwa na umri wa miaka saba mwaka 2010 kabla ya kuhamia Leverkusen akiwa na miaka 17, imeibuka na kueleza wazi na wao watafuatilia na watahakikisha wanapata mgao, hivyo Leverkusen wanataka kumuuza kwa bei kubwa ili wakigawana pesa isipungue sana.