Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Antony kawa mtamu balaa huko

Antony Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Kibrazili, Antony, 24, alionekana kuwa kimeo Manchester United, lakini amekuwa matata tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Hispania kwa mkopo dirisha la Januari, akitokea Old Trafford, ambako alikuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza.

MADRID, HISPANIA: WINGA, Antony amewasha moto huko Real Betis akifunga bao kwenye mechi ya pili mfululizo wakati miamba hiyo ilipokipiga na Gent kwenye mchakamchaka wa Europa Conference League.

Winga huyo wa Kibrazili, Antony, 24, alionekana kuwa kimeo Manchester United, lakini amekuwa matata tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Hispania kwa mkopo dirisha la Januari, akitokea Old Trafford, ambako alikuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza.

Antony alifunga kwenye mechi yake ya pili tu Betis kwenye mechi dhidi ya Celta Vigo wikiendi iliyopita, huku akiasisti kwenye mechi yake ya kwanza. Ameendeleza moto wake wa kutupia, akifunga bao maridadi kabisa dhidi ya Gent na kuufanya mkopo wake kuwa mtamu hadi sasa.

Kwenye kipindi cha pili, winga huyo alipokea mpira kwenye upande wa wingi ya kulia. Alikokota kidogo kuingia ndani, kabla ya kuachia shuti na kufunga kwenye kona ya chini ya goli.

Mashabiki haraka wakaanza kusema kitu kuhusu bao hilo la Antony na shabiki wa kwanza alisema: "United ilikuwa tatizo."

Mwingine alisema: "Sasa ipo wazi Man United inaharibu kila mchezaji."

Shabiki wa tatu alisema: "Maajabu ni kiasi gani mchezaji anayejiamini anachoweza kufanya."

Shabiki wa nne aliongeza: "Yule Antony bora amerudi."

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Real Betis, Ramon Alcaron ameshakiri timu yake ina mpango wa kumchukua Antony jumla mkopo wake utakapofika mwisho.

Antony aliondoka Man United akiwa na kadi nyingi za njano kuliko mabao aliyofunga baada ya usajili wake wa Pauni 86 milioni kutoka Ajax. Bado ana mkataba Old Trafford hadi Juni 2027.

Tangu dirisha la majira ya kiangazi 2022, Antony aliichezea Man United mara 96, amefunga mabao 12 na kuasisti mara tano.