Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shields ashuka uzani kumkabili Scott

SCOTT Pict

Muktasari:

  • Shields mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni bingwa wa dunia katika madaraja matano tofauti ataandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza pambano kuu katika ukumbi huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 16,888.

ATLANTA, MAREKANI: BINGWA wa dunia wa uzani wa Heavyweight Claressa Shields atashuka madaraja matatu ya uzani kupambana na bingwa wa uzani wa kati anayeshikilia mikanda ya WBC na WBA Kaye Scott katika pambano litakalopigwa Agosti 15 kwenye State Farm Arena, Atlanta, Marekani.

Shields atalazimika kupunguza uzito na kushuka kutoka heavyweight hadi middleweight ili kumkabili Scott.

Shields mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni bingwa wa dunia katika madaraja matano tofauti ataandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza pambano kuu katika ukumbi huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 16,888.

Scott wa Australia atakuwa akitetea mikanda yake ya WBC na WBA ya uzani wa kati aliyoitwaa Desemba mwaka jana baada ya kumshinda Olivia Curry.

SCOT 01

Akizungumzia pambano hilo, Shields alisema kila pambano analopigana kwa sasa lina lengo la kuacha historia.

“Katika hatua hii ya maisha yangu ya ndondi kila pambano linahusu urithi ninaoutengeneza. Kila pambano ni nafasi ya kuvuka mipaka ya kile kinachoonekana kinawezekana si kwa ajili yangu tu bali kwa ndondi za wanawake na kizazi kijacho kupitia Claressa Shields Promotions,” alisema.

Bingwa huyo wa zamani wa uzani wa kati alisema anamuheshimu Scott lakini lengo lake ni kurejea kuwa bingwa asiye na mpinzani.

“Kaye Scott ni bingwa na ninaiheshimu kazi aliyofanya. Lakini safari ya kuwa bingwa asiye na mpinzani tena katika uzani wa pauni 160 inaanza kwa kuwashinda mabingwa bora. Sijawahi kutafuta mapambano mepesi, siku zote nachagua mapambano yenye maana.”

SCOT 03

Mashabiki pia wanasubiri kuona pambano linaloweza kumkutanisha Shields na bingwa mwingine wa Olimpiki Lauren Price.

Mwezi Aprili mwaka huu ilitangazwa kuwa Price amesaini mkataba wa mapambano mawili unaotarajiwa kuhitimishwa kwa pambano dhidi ya Shields.

Shields alisema pambano dhidi ya Price linaweza kupigwa mwishoni mwa mwaka huu baada ya kumaliza majukumu yake dhidi ya Scott.

Alieleza kuwa pambano la Agosti 15 si la kuwania ubingwa pekee bali pia ni sehemu ya kuendeleza jitihada za kukuza ndondi za wanawake duniani.

“Atlanta ni fursa kubwa kwetu. Tulionyesha uwezo wa ndondi za wanawake huko Detroit. Tumejaza kumbi na kuunda matukio ambayo watu bado wanayakumbuka. Sasa ni wakati wa kuleta nguvu hiyo Atlanta,” alisema.

Promota Ben Shalom alisema mipango ni kuhakikisha wawili hao wanakutana mara mbili, pambano la kwanza likipigwa Marekani kabla ya marudiano nchini Wales.

Iwapo atamshinda Scott, Shields ataendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza pambano lolote na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kukutana na Lauren Price.

SCOT 02

REKODI ZAO

Licha ya pambano hilo kubeba mvuto wa aina yake, mabondia hao wameandika historia tofauti katika ndondi za wanawake.

Shields anatajwa kuwa mmoja wa mabondia wakubwa zaidi kuwahi kutokea, huku Scott akijijengea heshima kupitia uzoefu wake mkubwa licha ya kuwa na miaka 42.

Shields alianza kung’ara kwenye ngumi za ridhaa na kutwaa medali mbili za dhahabu za Olimpiki mwaka 2012 na 2016.

Baada ya kuhamia ngumi za kulipwa aliandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutwaa ubingwa usiopingika katika madaraja mawili tofauti ya uzani.

Mpaka sasa ana rekodi ya mapambano 18 akishinda yote na ni bingwa wa dunia katika madaraja matano tofauti.

Scott alipata umaarufu kupitia ngumi za ridhaa kabla ya kuhamia kulipwa. Desemba mwaka jana alimshinda Olivia Curry na kutwaa mikanda ya WBA na WBC ya uzani wa kati akiwa na miaka 42.

Shields anaingia ulingoni akiwa hajawahi kupoteza pambano lolote la kulipwa na akisaka kurejea kuwa bingwa asiye na mpinzani, huku Scott akitaka kutumia uzoefu wake kutetea mikanda yake dhidi ya mmoja wa mabondia bora kuwahi kutokea.