Wiki ya lawama League 1

Muktasari:

  • Wikiendi hii Serie A itakuwa inatimiza mzunguko wa 36 ambapo zitabaki mechi mbili kwa kila timu kasoro Atalanta na Fiorentina ambazo zitabakisha mechi tatu.

MILAN, ITALIA: NDIO. Ni wiki ya lawama kwa Napoli, Lazio na Fiorentina ambazo hazina uhakika wa kufuzu michuano ya kimataifa msimu ujao.

Wikiendi hii Serie A itakuwa inatimiza mzunguko wa 36 ambapo zitabaki mechi mbili kwa kila timu kasoro Atalanta na Fiorentina ambazo zitabakisha mechi tatu.

Kama timu yoyote itapoteza kati ya hizo tatu itapoteza mechi wikiendi, basi kutakuwa na kazi kubwa ya kufanya katika mechi mbili zitakazosalia na tatu kwa Fiorentina.

Hadi sasa Napoli inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 51, eneo ililopo kama itamaliza ligi hapo itakuwa imefuzu michuano ya Conference League, lakini changamoto ni kwamba Fiorentina iliyo nafasi ya tisa ina pointi 50 na bado ina mchezo mmoja mkononi, hivyo ikishinda huo itakuwa imeishusha Napoli kwa tofauti ya alama mbili.

Kwa maana hiyo Napoli ambayo ina mchezo mgumu leo dhidi ya Bologna utakaopigwa saa 1:00 usiku kama ikipoteza inaweza kushushwa na kuvukwa kwa pointi tano zaidi kwani ikiwa Fiorentina itashinda kiporo na mechi yake ya 36, basi itakuwa na pointi 56 wakati Napoli ikibakiwa na zilezile 51.

Lazio iliyo nafasi ya saba  inapambana kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa kumaliza nafasi tano za juu.

Kwa sasa ina alama 56, kupoteza kwao mechi ijayo inaweza kuwa pigo kubwa kwani timu inayoshika nafasi hiyo ya tano ambayo Atalanta ina pointi 60 tu, hivyo utofauti wao ni alama nne.

Ikiwa itapoteza halafu Atalanta ikashinda rasmi Lazio itakuwa imejiondoa katika kufuzu Ligi ya Mabingwa vita ikibaki kwa Roma na Atalanta ambazo zote zina pointi 60, Roma ikiwa nafasi ya sita na Atalanta ya tano.

Kivyovyote mechi za wikiendi hii zitakuwa ni za lawama kwa wachezaji kwani ukikosea tu, unakuwa umiweka timu katika mazingira magumu katika mapambano ya kitu inachohitaji.