Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wayne Rooney mambo safi, kutua Everton wiki hii

Muktasari:

Manchester United pia imetangaza kutega Pauni 20 milioni kwa ajili ya kudaka saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Oliver Giroud.

London, England. Mshambuliaji wa Manchester United, Wyne Rooney wiki hii anatarajiwa kutua kwenye klabu yake ya zamani ya Everton na ataendelea kulipwa mshahara wake wa awali wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Manchester United pia imetangaza kutega Pauni 20 milioni kwa ajili ya kudaka saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Oliver Giroud.

Rooney mwenye miaka 31 huyupo kwenye kikosi cha Manchester United ambacho kitatua Marekani Jumapili wiki hii ikiwa ni ziara yao kabla ya msimu kuanza.

Taarifa zilizopatikana klabuni hapo jana Jumanne, mipango yote ya uhamisho wa Rooney tayari imekamilika kwa uhamisho wa Pauni 26.5 milioni.