Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis Enrique aikejeli kijanja EPL

LUIS Pict

Muktasari:

  • Kikosi chake anachokinoa cha PSG kimetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano baada ya kuitupa nje Arsenal.

PARIS, UFARANSA: KOCHA wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique amekejeli kauli ya kwamba Ligue 1 ni ligi ya ‘wakulima’ licha ya kuzichapa timu nne za Ligi Kuu England kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kikosi chake anachokinoa cha PSG kimetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano baada ya kuitupa nje Arsenal.

Baada ya kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Emirates wiki iliyopita, ilimaliza kwa kushinda 2-1 katika mechi ya marudiano iliyofanyika Parc des Princes huko Ufaransa usiku wa Jumatano.

Ushindi dhidi ya Arsenal umeifanya PSG kuweka rekodi ya kipekee kabisa ya kuzichapa timu nne za Ligi Kuu England kwenye michuano ya Ulaya msimu huu.

Mabingwa hao wa Ligue 1 waliichapa Manchester City kwenye hatua ya ligi, huku ikitamba pia mbele ya Liverpool, Aston Villa na Arsenal. Na akizungumza baada ya mechi, Enrique alisema kwa kejeli kwamba Ligue 1 ilikuwa ligi ya wakulima, maneno ambayo yamekuwa yakitolewa kama dhihaka na watu wasioshawishika na ubora wa ligi hiyo ya Ufaransa.

Kocha Enrique alisema: “Hii ina maana kubwa, kila mtu ana ndoto za kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lengo letu la kwanza tulipotua Paris ilikuwa kutengeneza historia na sasa tupo kwenye mwelekeo mzuri.”

Alisema: “Ligi ya wakulimaa, sivyo? Sisi ni ligi ya wakulima. Lakini, ni si freshi. Tunafurahia matokeo na kila mtu anazungumzia timu yetu, sisi ni vijana, akili yetu, malengo yetu na jinsi tunavyocheza soka. Ni safi. Nimewapongeza wachezaji wangu kwa sababu ni bora.”

Kwenye fainali ya PSG itakwenda kukipiga na Inter Milan baada ya miamba hiyo ya Italia kuisukuma nje Barcelona kwenye hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 7-6. Kipute cha fainali kitapigwa Mei 31 huko Munich, Ujerumani.