Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano tayari Man United

MAN UTD Pict
MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Mchezaji mwingine anayeweza kuondoka wiki kadhaa zijazo ni winga mwenzake Antony, ambaye anatakiwa kurejea tena Real Betis ya La Liga.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim tayari amewapa ujumbe wa kutafuta timu nyingine mastaa watano wa miamba hiyo ya Old Trafford akiwamo Jadon Sancho anayetajwa ndiye atakuwa wa kwanza kuondoka.

Mchezaji mwingine anayeweza kuondoka wiki kadhaa zijazo ni winga mwenzake Antony, ambaye anatakiwa kurejea tena Real Betis ya La Liga.

Juventus inapambana kutaka kufanikisha dili la kumnasa Sancho, ambaye hajacheza mechi yoyote ya ushindani na Man United tangu alipopishana na Kocha Erik ten Hag, miaka miwili iliyopita wakati akiinoa timu hiyo.

Nyota huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 25 inadaiwa ana nia ya kuhamia Italia, licha ya kuhitajika pia na timu za Uturuki.

Sancho aliitumikia Chelsea kwa mkopo msimu uliopita, lakini timu hiyo haikuamua kumnunua jumla kwa Pauni 25 milioni zilizohitajika.

Man United bado inataka dau kama hilo ikiwa timu yoyote inamhitaji kiasi ambacho sio kikubwa sana lakini changamoto inaonekana kuwa katika mshahara kwani Sancho anahitaji Pauni 7 milioni kwa mwaka.

Sancho amekuwa na kipindi kigumu katika miaka minne   Old Trafford tangu aliposajiliwa kwa dau la Pauni 73 milioni kutoka Borussia Dortmund mwaka 2021.

Kwa upande mwingine, Real Betis inatarajia kufikia makubaliano ya kumrejesha Antony baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa kwa mkopo.

Mchezaji huyo amekuwa na maisha mazuri Hispania msimu uliopita na alikaa huko wakati wa mapumziko ya msimu.

Hadi sasa, hakuna timu nyingi zilivyoonyesha nia ya kumnasa Antony, jambo linalowapa matumaini Manuel Pellegrini na Betis yake kuwa watampata.

Mastaa wengine ambao Amorim ameshawasiliana nao ni Marcus Rashford, Alejandro Garnacho na Tyrell Malacia ambao pia wapo katika mpango wa kujiunga na timu nyingine.