Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Senegal abwaga manyanga akiweka sharti moja

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Pape Gueye amecheza mechi za Senegal katika Kombe la Dunia 2026, akifunga mabao mawili na kupiga pasi moja ya mwisho.

Kiungo wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya Villarreal ya nchini Hispania, Pape Gueye, ametangaza kujiweka kando kuichezea timu hiyo ikiwa ni saa chache tu baada ya miamba hiyo ya Afrika Magharibi kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 kufuatia kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Ubelgiji.

Gueye ameweka wazi kuwa hatarejea tena kuitumikia Senegal iwapo benchi la sasa la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu, Pape Thiaw, litaendelea kusalia madarakani.

Katika tamko lake, Gueye amesisitiza kuwa atapumzika kuichezea timu hiyo ya taifa kwa muda wote ambao benchi hilo litakuwa likiiongoza timu.

Ingawa kiungo huyo ameshindwa kuanika hadharani chanzo cha msuguano kati yake na viongozi hao wa benchi la ufundi, amewatoa hofu mashabiki na kuahidi kuvunja ukimya wake hivi karibuni ili kuujulisha umma sababu zilizokwamisha safari ya timu hiyo katika mashindano ya mwaka huu.

Cheche za mgogoro huo zilionekana dhahiri uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya 32 bora uliopigwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Julai 2, 2026, ambapo dakika ya 66 ya mchezo huo, benchi la ufundi lilifanya mabadiliko kwa kumtoa Gueye na kumwingiza Lamine Camara.

Uamuzi huo haukumfurahisha hata kidogo kiungo huyo ambaye alionyesha hasira za wazi kwa kukataa kupeana mkono na kocha Pape Thiaw, huku akielekea benchi la akiba wachezaji wa akiba kwa dharau ambapo wenzake walilazimika kuanza kumtuliza.

Kabla ya kuondolewa kwa timu yake, Gueye alikuwa mmoja wa nguzo muhimu za Senegal katika Fainali hizo za Kombe la Dunia, ambapo alifanikiwa kucheza mechi nne, akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Senegal imeondolewa kwa namna ya kushangaza baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 84, kabla ya kuruhusu Ubelgiji kusawazisha katika dakika tano za mwisho na kisha kufunga bao la ushindi dakika ya 120 ya muda wa nyongeza, na kuzika kabisa ndoto za Waafrika hao.