Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia wataka kumalizana na Salah mapema

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa mabosi hao ambao wanahitaji Salah aende kuitumikia Al-Ittihad ya  nchini humo, wanataka kufanya makubaliano kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia.

MATAJIRI wa Ligi Kuu Saudi Arabia, wana matumaini makubwa ya kuipata huduma ya mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa mabosi hao ambao wanahitaji Salah aende kuitumikia Al-Ittihad ya  nchini humo, wanataka kufanya makubaliano kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia.

Inaaminika sasa wakala wa Salah anazungumza na waarabu hao ambao wapo tayari kulipa mshahara wa hadi Pauni 60 milioni kwa mwaka ili tu fundi huyo akubali kujiunga nao.

Salah mwenye umri wa miaka 33, alitangaza kuondoka Liverpool mwezi uliopita  ikiwa ni baada ya kudumu kwa takribani miaka 10 akiwa na majogoo hao.

Liverpool ipo tayari kumwachia bure bila ya kudai ada ya uhamisho licha ya kuwa bado ana mkataba unaomalizika mwisho wa msimu ujao.

Baadhi ya timu Ulaya ikiwemo PSG zimeonyesha nia ya kumsajili fundi huyu lakini kwa sasa Waarabu ndio wanaonekana kushikilia mpini.


Jack Grealish

EVERTON in matumaini makubwa ya kumsainisha mkataba wa moja kwa moja winga wa Manchester City na timu ya taifa ya  England, Jack Grealish, 30, ambaye msimu huu anacheza kwa mkopo katika kikosi chao. Inaelezwa mabosi wa Everton wamevutiwa sana na kiwango ambacho Grealish amekionyesha tangu ajiunge nao na wanataka kumpa ofa ya mkataba wa moja kwa moja.


Dani Olmo

MANCHESTER City, Paris St-Germain na Arsenal zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Dani Olmo mwenye umri wa miaka , 27. Taarifa kutoka Barca zimefuchua mabosi wa timu hiyo wapo tayari kumuuza Olmo ikiwa watapokea ofa nono mwisho wa msimu. Olmo ambaye ni zao la akademi ya Barcelona, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Enderson

ATLETICO Madrid ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha dili la kiungo wa Atalanta na timu ya taifa ya Brazil, Ederson, 26. Katika mchakato wa kumsajili Atletico inakutana na ushindani mkali kutoka kwa Manchester United na Manchester City. Ederson ambaye amekuwa akifanya vizuri katika Serie A tangu msimu uliopita, mkataba wake wa sasa na Atalanta unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Elliot Aderson

MANCHESTER United inataka kusajili viungo wawili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na hadi sasa viungo wa kimataifa wa England, Elliot Aderson, 23, kutoka Nottingham Fores  staa wa Crystal Palace, Adam Wharton, 22, na kiungo wa  Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali ni miongoni mwa mastaa ambao imewaweka katika rada za kutaka kuwasajili.


Bernado Silva

KIUNGO wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno,  Bernardo Silva ambaye hivi karibuni ameripotiwa kuwa na mpango wa kuondoka kama mchezaji huru ifikapo mwisho wa msimu, hadi sasa bado hajafanya uamuzi wa timu gani atajiunga nayo ingawa Barcelona imeonyesha sana nia ya kumsajili. Inadaiwa Silva anataka kumaliza Kombe la Dunia kwanza kabla ya kuamua ni timu gani ajiunge nayo.


Karim Adeyemi

BARCELONA inamfuatilia mshambuliaji wa  Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani,  Karim Adeyemi mwenye umri wa miaka 24.

Vigogo hao wa Nou Camp wameshatuma hadi maskauti wao kwa ajili ya kumtazama Adeyemi. Hata hivyo, hawaonekani kuwa na uwezo wa kumsajili staa huyo kwa sasa kutokana na hali yao ya kiuchumi. Dortmund huenda ikahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni kumuuza staa huyu.


Crysencio Summerville

MSHAMBULIAJI wa West Ham na timu ya taifa ya Uholanzi, Crysencio Summerville, 24, yupo katika rada ya vigogo kadhaa Ulaya wanaohitaji kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsajili staa huyu ni Aston Villa, Everton, Tottenham, Marseille na Napoli. Timu nyingi zimevutiwa na kiwango cha Summerville alichoonyesha tangu msimu uliopita licha ya West Ham kutofanya vizuri.