Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu waingilia dili la Arsenal kwa Sesko

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Arsenal imekuwa ikiiwinda huduma ya staa huyu tangu Januari mwaka huu lakini imekuwa ikikwama kukamilisha dili lake kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na Leipzig pamoja na mchezaji mwenyewe.

MSHAMBULIAJI wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Slovenia, Benjamin Sesko, mwenye miaka 22, ambaye pia anawindwa na Arsenal ameripotiwa kuwa katika rada za Al-Hilal ya Saudi Arabia inayohitaji kumsajili katika dirisha hili.

Arsenal imekuwa ikiiwinda huduma ya staa huyu tangu Januari mwaka huu lakini imekuwa ikikwama kukamilisha dili lake kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na Leipzig pamoja na mchezaji mwenyewe.

Al-Hilal inadaiwa kuwa tayari kutoa ada ya uhamisho ya Euro 100 milioni inayohitajika na Leipzig, pia inataka kumpa Sesko mshahara unaofikia mara tatu ya ule ambao anaupata kwa sasa.

Msimu uliopita Sesko ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2029, alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 21.

Hata hivyo, Al-Hilal imepanga mpango mbadala ikiwa wa kugeuka kwa mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa Jean-Philippe Mateta, mwenye miaka 28.

Inaelezwa Leipzig haina shida yoyote katika kumuuza Sesko katika dirisha hili ikiwa tu timu inayomhitaji itaweka mezani kiasi cha pesa kinachohitajika.

Sesko mwenyewe anadaiwa kuwa anatamani sana kucheza Ligi Kuu England msimu ujao lakini hatolazimisha kuondoka kwa sasa.

Baada ya kukosa matajji ya Ligi Kuu England kwa miaka mingi, Arsenal inataka kutengeneza kikosi matata kabisa cha kuiwezesha kuwa wababe.


Jordan Henderson

KIUNGO mkongwe wa aliyewahi kutamba na miamba ya Jiji la Liverpool ya Ligi Kuu England, Jordan Henderson, 35, anatarajia kuondoka Ajax katika dirisha hili la majira ya baridi baada ya kuitumikia timu hiyo kwa  msimu mmoja na nusu. Hata hivyo, haijajulikana ni wapi staa huyu atakwenda kwani dili lake la kwenda Monaco limefeli ingawa ripoti zinaeleza anaweza kurudi Englnd. Tangu aondoke Liverpool hajawa na kiwango kizuri alikokwenda.


Noni Madueke

ARSENAL imeshafikia makubaliano binafsi na winga wa Chelsea, Noni Madueke kwa ajili ya kumsajili dirisha hili na sasa inafanya mazungumzo na Chelsea kwa ajili ya kukubaliana ada ya uhamisho. Madueke ni mmoja kati ya mastaa wa Chelsea waliokuwa wakilalamikiwa sana na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango chake uwanjani. Mkataba wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Renato Veiga

KWA mujibu wa gazeti la  BILD, kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany amependekeza jina la beki wa kushoto wa Chelsea, Renato Veiga na anataka asajiliwe katika dirisha hili. Veiga, 21, alijiunga na kikosi cha Kocha Enzo Maresca katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi na alisaini mkataba wa miaka saba katika dili lililoigharimu  Chelsea Euro 14 milioni.


Neil El Aynaoui

SUNDERLAND, Leeds United na Wolves zinapambana kumsajili kiungo wa kati wa Lens na timu ya taifa ya Morocco, Neil El Aynaoui, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka AS Roma, Juventus na AC Milan ambazo pia zinahitaji saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. Hata hivyo, ripoti zinadai Neil mwenyewe anatamani sana kwenda kucheza Ligi Kuu England kwa sababu ni ndoto yake.


James McAtee

NOTTINGHAM Forest na Crystal Palace ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu England zinazofikiria kumsajili kiungo wa Manchester City, James McAtee,  22, katika dirisha hili la usajili. Taarifa za kuaminika kutoka tovuti ya Sky Sports zimefichua Man City ipo tayari kumtoa mchezaji huyo lakini kwa mkopo sio kumuuza mazima.


Evan Ferguson

BRIGHTON iko tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ireland, Evan Ferguson, mwenye miaka 20, kwenda Roma katika dirisha hili. Licha ya utayari wao, hadi sasa Roma bado haijafikia makubaliano na wawakilishi wa Evan mwenyewe na mazungumzo bado yanaendelea.



El Hadji Malick Diouf

KOCHA wa Slavia Prague, Jindrich Trpisovsky, amethibitisha El Hadji Malick Diouf yuko mbioni kuondoka kwenye timu yake dirisha hili jambo linalozidisha tetesi staa huyo ni kweli anaweza kutua England ambako anahusishwa na timu mbalimbali kama West Ham na Leeds United.

Beki huyu wa kimataifa wa Senegal ana umri wa miaka 20.