Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe anavyomtishia  Messi kiatu cha dhahabu

Muktasari:

  • Wakati huohuo, Vinicius Jr na Erling Haaland nao wanaendelea kutoa ushindani mkali katika kinyang’anyiro hicho, huku nyota wakubwa wakiendelea kung’ara katika mashindano, lakini hakuna aliyekuwa na ushawishi mkubwa kama Messi.

NEW YORK, MAREKANI: MBIO za kuwania Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot) katika Kombe la Dunia 2026 zimeingia katika hatua ya kusisimua kuelekea michezo ya mtoano, huku Kylian Mbappe akimfikia Lionel Messi kileleni mwa orodha ya wafungaji bora.

Wakati huohuo, Vinicius Jr na Erling Haaland nao wanaendelea kutoa ushindani mkali katika kinyang’anyiro hicho, huku nyota wakubwa wakiendelea kung’ara katika mashindano, lakini hakuna aliyekuwa na ushawishi mkubwa kama Messi.

Baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) dhidi ya Algeria, nahodha huyo wa Argentina aliongeza mawili dhidi ya Austria, akionyesha tena uwezo wake mkubwa wa kurejea kwa nguvu hata baada ya kukosa penalti. Baadaye aliingia akitokea benchi na kufunga tena dhidi ya Jordan, jambo lililoonekana kuwa la kawaida kwake.

Kwa upande mwingine, Mbappe ameendelea kuwa moto mbele ya lango, ambapo mabao yake mawili dhidi ya Sweden yaliisaidia Ufaransa juzi kushinda 3-0 na kutinga hatua ya 16 bora, huku mshambuliaji huyo akiendelea kuthibitisha uwezo wake wa kung’ara katika mashindano makubwa.

Ushindi huo pia ulimpandisha kileleni mwa orodha ya wafungaji, akiwa amefunga mabao sita sawa na Messi, lakini akitangulia kutokana na kuwa na pasi mbili za mabao.

Naye Haaland aliendeleza rekodi yake ya kufunga katika mechi ya 13 mfululizo za kimataifa baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 86 dhidi ya Ivory Coast katika hatua ya 32 bora, na kuipeleka Norway katika raundi inayofuata.

Bao hilo lilimfikisha mabao matano katika mashindano hayo ikiwa moja nyuma ya Messi na Mbappe. Harry Kane ambaye jana alikuwa uwanjani dhidi ya DR Congo pia bado yupo katika mbio hizo baada ya kufunga kwa kichwa dhidi ya Panama katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa England.

Vinicius Jr naye aling’ara kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Scotland, huku Ousmane Dembele akiweka wazi dhamira yake ya kuwania tuzo hiyo baada ya kufunga hat-trick ya kuvutia dhidi ya Norway.

Kwa mujibu wa kanuni za Kombe la Dunia, ikiwa wachezaji watamaliza mashindano wakiwa na idadi sawa ya mabao, mshindi wa Kiatu cha Dhahabu ataamuliwa kwa kuzingatia idadi ya pasi za mabao.

Endapo sare itaendelea, kigezo kitakuwa dakika chache alizocheza na uwiano wa mabao kwa dakika alizotumia uwanjani.