Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vini Jr atuliza presha Real Madrid

Vini Pict
Vini Pict

Muktasari:

  • Vini Jr amebakiza miaka miwili tu kwenye mkataba wake wa sasa huko Real Madrid jambo lililoibua wasiwasi mkubwa endapo kama ataendelea kubaki Bernabeu.

MADRID, HISPANIA: SUPASTAA wa Kibrazili, Vinicius Junior amesema anataka kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Real Madrid.

Vini Jr amebakiza miaka miwili tu kwenye mkataba wake wa sasa huko Real Madrid jambo lililoibua wasiwasi mkubwa endapo kama ataendelea kubaki Bernabeu.

Hilo limekuwa gumzo zaidi kutokana na klabu za Saudi Pro League kuweka mezani mkwanja wa maana na moja ya timu ya Mashariki ya Kati, iliipa Madrid ofa ya Pauni 200 milioni ili kumchukua staa huyo mwenye umri wa miaka 24.

Ada hiyo ingemfanya Vini Jr kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye historia ya mchezo wa soka. Lakini, yupo tayari kubaki zake kwenye kikosi hicho cha Carlo Ancelotti, ambacho kinafukuzia ubingwa wa La Liga msimu huu na kimetinga hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumenyana na Atletico Madrid kwenye hatua hiyo kuwania kutinga robo fainali.

Katika kuelekea mchezo huo wa Madrid Derby, Vinicius aliweka wazi mpango wake ni kubaki kwenye Jiji la Madrid, aliposema kwenye klabu hiyo anaishi ndoto zake.

"Nimekuwa mtulivu kwa sababu mkataba wangu utakwisha 2027 na natumaini nitasaini dili jipya haraka iwezekanavyo, kwa sababu nimekuwa na furaha kuwa hapa," alisema.

"Naishi ndoto zangu kwa kucheza na wachezaji bora duniani, kocha bora, rais bora na mashabiki bora. Hapa kila mtu ananipenda sana. Nisingekuwa kwenye nafasi bora zaidi ya hii. Ndoto za utoto wangu ilikuwa kuja hapa. Sasa nimefanikiwa kufika hapa, naandika historia yangu.

"Nimeshinda, lakini bado naendelea kushinda ili kuingia kwenye historia ya klabu. Hiyo ni heshima kubwa kwa wachezaji bora waliowahi kupita hapa, magwiji na mimi nataka kuwa kama wao."

Vinicius alifunga bao kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopita na anataka kushinda tena taji hilo msimu huu.