Vigogo EPL waiteka UEFA
Muktasari:
- Arsenal, Liverpool, Tottenham, Chelsea na Man City zimefuzu bila kuhitaji kucheza mechi za mchujo lakini Newcastle itakutana na aidha Monaco au Qarabag ili kuwania nafasi ya kwenda hatua ya 16 bora.
LONDON, ENGLAND: HATUA ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imemalizika na timu tano za Ligi Kuu England zimefuzu moja kwa moja hatua ya mtoano baada ya kumaliza nafasi za juu.
Arsenal, Liverpool, Tottenham, Chelsea na Man City zimefuzu bila kuhitaji kucheza mechi za mchujo lakini Newcastle itakutana na aidha Monaco au Qarabag ili kuwania nafasi ya kwenda hatua ya 16 bora.
Droo ya mchujo, itakayofanyika leo, saa 8:00 mchana huko Switzerland, itajumuisha vigogo kadhaa akiwemo mabingwa watetezi Paris Saint-Germain, Real Madrid, Juventus na Inter Milan ambao wote wameshindwa kufuzu moja kwa moja.
Chelsea sasa inaweza kukutana na Newcastle katika hatua ya 16 bora –ikiwa timu hiyo itapita katika mtoano ingawa pia kuna uwezekano ikakutana na PSG.
Arsenal ambayo imeshinda mechi zote za hatua ya awali za michuano hii kwa msimu huu, inatarajia kukutana na moja kati ya Atalanta, Bayer Leverkusen, Borussia Dortmund au Olympiacos.
Liverpool ilimaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Qarabag na inatarajiwa kukutana na aidha Juventus, Atletico Madrid, Club Brugge au Galatasaray.
Wapinzani hao hao pia wanaweza kukutana na Tottenham, ambayo ilifuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 bora baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Eintracht Frankfurt.
Man City ya Pep Guardiola iliingia kwa tabu 16 bora ikimaliza nafasi ya nane baada ya kuichapa Galatasaray mabao 2-0 ambapo Erling Haaland na Rayan Cherki walifunga bao moja moja kila mmoja.
Man City ililazimika kusubiri hadi mwisho wa mechi kati ya huku Benfica ya Jose Mourinho na Real Madrid ambayo ilimalizika kwa Madrid kupotez kwa mabao 4-2, hivyo kupishana kwa tofauti ya mabao kati yao na vijana hao wa Pep Guardiola.
Kipa wa Benfica, Anatoliy Trubin, alifunga bao la kichwa cha kuzima kabisa matumaini ya Madrid iliyokuwa ikihitaji walau sare ili kupata nafasi ya kufuzu moja ka moja katika hatua inayofuata.
Katika hatua ya 16 bora, Man City inaweza kukutana na Madrid, Inter Milan, Bodo Glimt au Benfica.
MSIMAMO ULIVYO
Arsenal iliongoza msimamo baada ya kushinda mechi zote za hatua ya ligi, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Bayern Munich, Liverpool ya tatu Tottenham ya nne.
Timu zilizomaliza nafasi ya tisa hadi ya 24 zitapambana kuwania nafasi za 16 bora kupitia mechi za mchujo.
Newcastle ndiyo timu pekee ya England iliyoingia mchujo na inaambatana na vigogo wa Ulaya PSG, Real Madrid, Inter na Juventus.
Timu zilizomaliza chini ya nafasi ya 24 zinaondolewa kabisa kwenye mashindano hayo.
16 BORA ITAKUWAJE
Arsenal vs Atalanta / Leverkusen / Dortmund / Olympiacos
Bayern Munich vs Atalanta / Leverkusen / Dortmund / Olympiacos
Liverpool vs Juventus / Atletico Madrid / Club Brugge / Galatasaray
Tottenham vs Juventus / Atletico Madrid / Club Brugge / Galatasaray
Barcelona vs PSG / Newcastle / Monaco / Qarabag
Chelsea vs PSG / Newcastle / Monaco / Qarabag
Sporting vs Real Madrid / Inter / Bodo/Glimt / Benfica
Man City vs Real Madrid / Inter / Bodo/Glimt / Benfica
RATIBA YA MECHI ZA MCHUJO
Mechi za mkondo wa kwanza wa mchujo zitachezwa Februari 17 na 18, huku za marudiano zikipigwa kati ya Februari 24 hadi 25 na hapa ni namna ambavyo droo itakuwa.
Real Madrid vs Bodo/Glimt / Benfica
Inter vs Bodo/Glimt / Benfica
PSG vs Monaco / Qarabag
Newcastle vs Monaco / Qarabag
Juventus vs Club Brugge / Galatasaray
Atletico Madrid vs Club Brugge / Galatasaray
Atalanta vs Dortmund / Olympiacos
Leverkusen vs Dortmund / Olympiacos
Dortmund vs Atalanta / Leverkusen
Olympiacos vs Atalanta / Leverkusen
Club Brugge vs Juventus / Atletico Madrid
Galatasaray vs Juventus / Atletico Madrid
Monaco vs PSG / Newcastle
Qarabag vs PSG / Newcastle
Bodo/Glimt vs Real Madrid / Inter Milan
Benfica vs Real Madrid / Inter Milan