Madrid, PSG zasubiri mchujo UEFA
Muktasari:
- Timu zilizofuzu moja kwa moja 16 Bora ni zilizomaliza ndani ya nane bora katika hatua ya ligi ambazo ni Arsenal, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting Lisbon na Manchester City. Hata hivyo, bado haijajulikana zitapangwa dhidi ya timu zipi katika hatua ya mtoano.
JANA usiku, zimepigwa mechi 18 za Ligi ya Mabingwa Ulaya kuhitimisha mfumo wa ligi ambapo sasa zimefahamika timu nane zilizofuzu moja kwa moja hatua ya 16 Bora, huku zingine 16 zikisubiri kucheza mtoano ili zifuzu zikiwamo Real Madrid, PSG na Inter Milan.
Timu zilizofuzu moja kwa moja 16 Bora ni zilizomaliza ndani ya nane bora katika hatua ya ligi ambazo ni Arsenal, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting Lisbon na Manchester City. Hata hivyo, bado haijajulikana zitapangwa dhidi ya timu zipi katika hatua ya mtoano.
Timu zilizomaliza nafasi ya 9 hadi 24 kwenye hatua ya ligi, zitachuana katika mechi za nyumbani na ugenini ili kupata washindi nane watakaofuzu kwenda hatua ya 16 bora.
Kulingana na nafasi walizomaliza kwenye ligi, timu ya 9 na 10 zitacheza dhidi ya moja kati ya timu za 23 au 24. Timu ya 11 na 12 zitakutana na moja kati ya timu za 21 au 22. Mfumo huu unaendelea kwa mpangilio huo hadi kukamilisha mchujo huo.
Kwa mfano, Real Madrid (nafasi ya 9) na Inter Milan (nafasi ya 10) zitakutana na moja kati ya Bodo/Glimt au Benfica (nafasi ya 23 na 24). Ni droo ya mtoano itakayoamua nani atacheza na nani hasa.
Ni muhimu kutambua kuwa, timu kutoka nchi moja zinaweza kukutana katika hatua hii, huku pia timu zilizokutana tayari kwenye hatua ya ligi pia zinaweza kupangwa tena.
Droo ya mtoano itafanyika katika makao makuu ya UEFA nchini Uswisi, kesho Ijumaa, Januari 30, 2026 kuanzia saa 8:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Mechi za mtoano zitachezwa katika wiki za katikati ya Februari 2026 ambapo mechi za mkondo wa kwanza ni Februari 17 na 18 na marudiano Februari 24 na 25.
Baada ya kukamilika kwa mechi hizo za mtoano, droo ya hatua ya 16 bora, robo fainali na nusu fainali itafanyika Februari 27, 2026.
ZITAKAZOCHEZA MTOANO
Nafasi ya 9: Real Madrid
Nafasi ya 10: Inter Milan
Nafasi ya 11: PSG
Nafasi ya 12: Newcastle
Nafasi ya 13: Juventus
Nafasi ya 14: Atletico Madrid
Nafasi ya 15: Atalanta
Nafasi ya 16: Bayer Leverkusen
Nafasi ya 17: Borussia Dortmund
Nafasi ya 18: Olympiakos
Nafasi ya 19: Club Brugge
Nafasi ya 20: Galatasaray
Nafasi ya 21: Monaco
Nafasi ya 22: Qarabag
Nafasi ya 23: Bodo/Glimt
Nafasi ya 24: Benfica
MATOKEO MECHI ZA JANA
Ajax 1–2 Olympiacos
Arsenal 3–2 Kairat
Monaco 0–0 Juventus
Bilbao 2–3 Sporting CP
Atlético 1–2 Bodø/Glimt
Leverkusen 3–0 Villarreal
Dortmund 0–2 Inter Milan
Club Brugge 3–0 Marseille
Frankfurt 0–2 Tottenham
Barcelona 4–1 Copenhagen
Liverpool 6–0 Qarabağ
Man City 2–0 Galatasaray
Pafos 4–1 Slavia Prague
PSG 1–1 Newcastle
PSV 1–2 Bayern
Union Saint-Gilloise 1–0 Atalanta
Benfica 4–2 Real Madrid
Napoli 2–3 Chelsea