Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Victoria: Mke wa bosi na yeye ni bosi

ATM Pict

Muktasari:

  • Rebekah na Coleen wamekuwa kwenye vita kali sana ya kutambiana. Lakini, wake hao wa mastaa wawili hao wa England, hawafui dafu kabisa kwa mrembo Victoria Adams, ambaye ni mke wa supastaa David Beckham.

MIAMI, MAREKANI: CHUKUA pesa za mke wa Wayne Rooney, Mrembo Coleen. Changanya na pesa za mke wa Jamie Vardy, mrembo Rebekah, weka pamoja. Unaambiwa hivi, bado hawamfikii na wameachwa kwa mbali sana.

Rebekah na Coleen wamekuwa kwenye vita kali sana ya kutambiana. Lakini, wake hao wa mastaa wawili hao wa England, hawafui dafu kabisa kwa mrembo Victoria Adams, ambaye ni mke wa supastaa David Beckham.

Rebekah utajiri wake unatajwa kuwa ni Dola 3.8 milioni, wakati Coleen ana pato la Dola 18.9 milioni.

ATM 01

Hicho ni kiwango kidogo sana kwa dada yao kwenye kundi la wake maarufu wa wanasoka duniani, Victoria, ambaye anaripotiwa kuwa na pato ya Dola 70 milioni.

Lakini, kutokana na kufanya biashara zake sambamba na mumewe, Beckham, pato la Victoria kwa pamoja la lile la mumewe linatajwa kuwa ni Dola 500 milioni.

Kwa mujibu wa The Sunday Times Rich List kwa mwaka 2024, familia hiyo ya Beckham iliripotiwa kuwa na pato la Dola 576 milioni. Hata hivyo, anayeleta kipato kwenye familia hiyo si Beckham, bali na mrembo Victoria pia, naye makusanyo yake yanaongeza pato la familia hiyo.

Kwa mwaka huu wa 2025, Victoria aliripotiwa kuingiza Dola 250 milioni. Kwenye dili zake mrembo huyo, mshahara wake unaripotiwa kuwa Dola 15 milioni kwa mwaka.

ATM 02

Anavyopiga pesa

Mrembo Victoria ni mfanyabiashara, mbunifu wa mitindo ya mavazi, mwanamitindo na mwimbaji pia. Alizaliwa Harlow, Essex, United Kingdom na kukulia Hertfordshire, kwa mama Jacqueline Doreen na baba Anthony William Adams, huku yeye akiwa mtoto mkubwa kwenye familia ya watoto watatu. Mama yake alifanyakazi kwenye kampuni ya bima na pia alikuwa mhudumu wa saluni, wakati baba yake alikuwa injia wa umeme na alikuwa na biashara ya kuuza vifaa vya jumla vya umeme.

Victoria ameingiza pesa kupitia biashara ya muziki, mitindo na dili nyingine za matangazo ya biashara. Victoria alikuwa kwenye kundi la muziki wa pop lililofahamika kwa jina la Spice Girls, huku yeye alikuwa akifahamika kwa jina la Posh Spice. Wakati kundi lao la muziki lilipokuwa juu kabisa, Victoria alikuwa akivuna hadi Dola 75 milioni kwa mwaka. Kundi hilo lilipokuwa kwenye ziara za kimuziki, aliingiza hadi Dola 70 milioni. Kupitia nembo yake ya mitindo na ile ya haki za taswira za mumewe, Victoria aliingia kwenye familia hiyo hadi Dola 24.3 milioni kati ya mwaka 2016 na 2017. Hiyo ilikuwa wastani wa kuvuna Dola 500,000 kwa mwezi.

Kundi la Spice Girls liliposambaratika, Victoria alikwenda kusaini kwenye lebo za Virgin Records na Telstar Records na kurekodi nyimbo nne. Rekodi yake ya kwanza kuitambulia “Out of Your Mind”, ilishika namba mbili kwenye chati za muziki za Uingereza. Alipiga pesa pia kwa kutengeneza filamu nne tofauti za maisha yake binafsi, ambazo zilimletea mezani dili kibao za matangazo ya kibiashara na kupiga mkwanja wa kutosha pamoja na blandi mbalimbali za mabegi ya akina mama.

ATM 05

Makazi na familia

Victoria na mumewe David, ambaye walioana Julai 4, 1999 kwenye harusi iliyogharimu Pauni 825,000 wakati huo - wamefanikiwa kupata watoto wanne; watatu wa kiume Brooklyn, Romeo, Cruz na mmoja wa kike, Harper Seven. Familia hiyo ya kitajiri inamfanya Victoria atambe tu, ambapo kwenye suala la makazi ataamua aende kuishi wapi kwa muda anaotaka. Familia hiyo ina miliki majumba Manchester kwenye mtaa wa matajiri Cheshire, huku jumba lao maarufu England ni lile lililopachikwa jina la  Beckingham Palace.

Lakini, ina makazi pia Palm Jumeirah, Dubai na ina miliki pia makazi ndani ya Burj Khalifa, Dubai - ambayo ilinunua kwa Dola 5 milioni. Familia hiyo ina jumba pia Beverly Hills, Marekani, Miami Beach, Lancashire, Saint Tropez, kusini mwa Ufaransa, Hispania, ambako kuna jumba lenye thamani ya Dola 3.7 milioni, La Moraleja. Familia hiyo inamiliki makazi pia Uholanzi na ina makazi ndani ya ghorofa lenye makazi ya kisasa kabisa huko Miami.

ATM 03

Usafiri upoje

Kwanza kabisa, Victoria na familia yake wanamiliki ndege binafsi, Bombardier Challenger 350, yenye uwezo wa kuchukua abiria 10 na kupaa kwa umbali wa maili 3,682 bila ya kuhitaji kujaza mafuta.

Ukiweka kando usafiri wa ndege binafsi ya familia, Victoria anatamba pia na boti mbili za kifahari, Madsummer na Seven, ambazo ni za familia hiyo ya Beckham. Madsummer ilinunuliwa kwa Dola 229 milioni na ina uwezo wa kuchukua watu 12, huku ndani kukuwa na chumba cha sinema, bwawa la kuogelea, jacuzzi, gym na eneo la watoto kucheza sambamba na spa na sauna. Ina vifaa vya kuvua samaki na michezo ya baharini. Seven ilinunuliwa kwa Pauni 16 milioni na yenyewe ina deki tatu, sio kubwa sana.

ATM 04

Kwenye ishu ya usafiri wa magari ya kifahari huko ndiyo balaa kabisa. Victoria anabadili tu magari kama nguo, maana kwenye maegesho yao kuna ndinga kibao za kifahari, kuanzia Jaguar F-Type Project 7, Aston Martin V8 Vantage, McLaren MP4-12C Spider, McLaren 720S, Lamborghini Gallardo, Maserati MC20, Bentley Continental GT Supersports, Bentley Mulsanne, Rolls-Royce Ghost, Rolls-Royce Phantom Drophead Coupe, Volkswagen Golf, Porsche 911 Carrera, Jaguar XK8, Ferrari 360 Spider, Ferrari 550 Maranello, Ferrari 612 Scaglietti, Jeep Wrangler, Range Rover Sport, Cadillac Escalade na Mercedes CLK.