Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Victor Osimhen aikataa Juventus

OSIMHEN Pict

Muktasari:

  • Victor Osimhen anacheza msimu wa 2024-25 akiwa kwa mkopo Galatasaray, amekuwa akitajwa kuwa hana mpango wa kutaka kuendelea kubakia katika timu hiyo wala Napoli na badala yake atajiunga na timu ya EPL.

TURIN, ITALIA: MAOMBI ya Juventus ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi yanadaiwa kukataliwa na staa huyo ambaye anatamani zaidi kutua England kweye moja kati ya timu kubwa.

Victor Osimhen anacheza msimu wa 2024-25 akiwa kwa mkopo Galatasaray, amekuwa akitajwa kuwa hana mpango wa kutaka kuendelea kubakia katika timu hiyo wala Napoli na badala yake atajiunga na timu ya EPL.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka JuveFC (kwa njia ya Football Italia), Osimhen, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, alikaribishwa na Juventus kujiunga nao kabla ya msimu wa 2025-26, lakini alikataa ofa hiyo kwa wakati huo.

Mbali ya kukataliwa, Juventus walirudi tena mezani kuzungumza na wawakilishi wake lakini bado msimamo wa straika huyo umeendelea kuwa vilevile.

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, Osimhen alifeli kujiunga na Chelsea katika dakika za mwisho za dirisha la usajili huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni maslahi.

Tangu wakati huo kumekuwa na kundi kubwa la timu ambazo zinahusishwa naye ndani ya England ambazo zinapata tabu katika eneo lao la ushambuliaji.

Katika mkataba wake ana kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka kwa Euro 75 milioni ambacho kinaweza kuanza kutumika mwisho wa msimu huu.

Juventus imekuwa ikitafuta mshambuliaji mzuri namba tisa kuelekea dirisha lijalo  ambapo wamepanga kumwachia Dusan Vlahovic ambaye benchi la ufundi haliliridhishwi na kiwango chake na hata baada ya kumpata Randal Kolo Muani kwa mkopo kutoka PSG bado hawaonekani kuwa na mpango wa kumsainisha mkataba mpya.

Mapema wiki hii, chapisho la kutoka tovuti ya CatalanSPORT liliripoti kwamba Osimhen anazungumza na Barcelona, ambao wanahitajika sana kumtafuta mrithi wa Robert Lewandowski ambaye umri unamtupa mkono.