Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba ni Misri au Uturuki

MISRI Pict


MABOSI wa Simba SC kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo wameanza mikakati ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26, ambapo imefahamika kuwa kambi imependekezwa tena kufanyika nje ya nchi ni ama Misri au Uturuki.


Uamuzi huo umetokana na mapendekezo ya benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ambaye inaelezwa amesisitiza umuhimu wa maandalizi kufanyika kwenye mazingira yatakayosaidia kujenga timu yenye ushindani zaidi ya msimu uliopita.


Kwa mujibu wa taarifa za ndani, kambi hiyo inatarajiwa kuanza rasmi Julai 25 mwaka huu, muda mfupi baada ya wachezaji na benchi lote la ufundi kurejea kutoka likizo. Tayari programu za mazoezi binafsi zimesambazwa kwa wachezaji wote ili kuhakikisha wanarejea kambini wakiwa katika hali bora ya kiafya na kimbinu.


Misri, Uturuki

Akizungumza na Mwanaspoti, mmoja wa maofisa wa juu kutoka ndani ya benchi la ufundi wa Simba, ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini, alisema: “Tumechagua Misri na Uturuki kama chaguo la kwanza kwa sababu ya mazingira yao bora ya maandalizi. Misri ina klabu nyingi zinazoshiriki mashindano ya Afrika na zina miundombinu bora, wakati Uturuki inatoa hali ya hewa nzuri, viwanja vya kisasa na nafasi ya kucheza mechi za kirafiki na timu kutoka Ulaya Mashariki na Asia. Tunahitaji kikosi chetu kiingie msimu mpya kikiwa tayari kabisa.”


Maandalizi

Fadlu ambaye aliiongoza timu hiyo hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, amewekewa wazi malengo mapya.  Malengo hayo mama ni kutwaa ubingwa wa ligi ambao watani zao wa jadi, Yanga wametwaa mara nne mfululizo na kufika angalau nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa ripoti ya kiufundi iliyowasilishwa kwa uongozi wa klabu, Fadlu ameomba kusajiliwa kwa wachezaji wapya wasiopungua sita katika nafasi ya beki wa kati, kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji, mshambuliaji wa kati, kipa mwenye uzoefu na winga wa kasi.

“Hatuwezi kwenda mbele zaidi kwa kutumia mfumo wa kusubiri mchezaji mmoja aumie ndipo tuanze kuhangaika. Tunahitaji kikosi chenye uwiano na uwezo wa kupambana mechi za ndani na nje ya nchi. Wachezaji wapya watasaidia sana hasa kwenye mzunguko wa mechi nyingi,” alisema mtoa taarifa kutoka idara ya ufundi.


Mechi za kirafiki

Katika kambi hiyo ya nje ya nchi, Simba inatarajiwa kucheza takribani mechi nne hadi tano za kirafiki dhidi ya timu kutoka ligi kubwa na zenye historia ya kimataifa, ambazo zitapangwa kwa kushirikiana na mawakala wa kimataifa wa michezo.

Lengo la mechi hizo si tu kuangalia viwango vya wachezaji wapya, bali kujaribu mifumo mipya ya uchezaji, kutengeneza muunganiko wa kikosi na kuwapa wachezaji changamoto kabla ya kuingia kwenye ratiba  ya mashindano.


Mabosi kazini

Wakati benchi la ufundi likijipanga upande wa maandalizi ya kambi, mabosi wa Simba hawajalala.

Kwa sasa wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa nyota wapya waliopendekezwa na Fadlu, huku vyanzo mbalimbali vikieleza kuwa mazungumzo na baadhi ya wachezaji yapo hatua nzuri.

Kumekuwa pia na mazungumzo na mawakala wa kimataifa wanaowakilisha wachezaji kutoka Afrika Magharibi na Kusini kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kuleta mastaa wenye sifa zinazohitajika.