Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugarte kajiweka kwa X wa Mbappe

Muktasari:

  • Cunha,ambaye alisajiliwa kwa Pauni 62.5 milioni kutoka Wolves alikuwa mchezaji wa kwanza kuripoti kambini kwenye viwanja hivyo vya mazoezi vya Man United, akiwasili kabla ya saa 2 asubuhi.

PARIS, UFARANSA: KIUNGO wa Manchester United, Manuel Ugarte amefichua kuzama kwenye mahaba na mrembo Georgia May Heath, ambaye ni X wa fowadi wa Real Madrid, Kylian Mbappe.

Ugarte, 24, amethibitisha hilo baada ya uvumi wa wiki kadhaa baada ya kutuma picha zao kwenye mtandao wa kijamii wakiponda raha katika kipindi cha likizo.

Ugarte alielekeza posti yake kwa mrembo Georgia May sambamba na emoji ya moyo kwenye posti ya picha inayowaonyesha wakiwa kwenye boti ya kifahari huko Hispania.

Mrembo Georgia May ni mwanamitindo na mhamasishaji wa masuala ya urembo, ana wafuasi karibu 230,000 kwenye Instagram na zaidi ya wafuasi 50,000 huko TikTok.

Aliwahi kuwa na uhusiano na Mbappe na walionekana wakiwa kwenye mahaba mazito, Januari 2024.

Lakini, Aprili mwaka huu uliibuka uvumi mrembo huyo mwenye maskani yake Uingereza na Australia - ameachana na penzi la Mbappe na kuhamia kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa PSG, Ugarte.

Na sasa imefahamika wazi kwamba Ugarte na mrembo Georgia May kuna kitu kinaendelea, huku Mbappe akiwa hana shida yoyote baada ya kubonyeza kitufe cha ‘like’ kwenye posti iliyopostiwa huko Instagram inayowaonyesha wapendanao hao.

Mashabiki wa Man United wanaamini uhusiano huo utampa mzuka Ugarte na kuonyesha kiwango bora msimu ujao. Ugarte alijiunga na Man United akitokea PSG mwaka jana kwa ada ya Pauni 43 milioni.

Huduma yake haikusaidia timu hiyo kwa msimu uliopita, ikimaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Na sasa Man United inafikiria mpango wa kuvamia tena PSG kwenda kunasa kiungo pacha wa Ugarte, Mhispaniola Fabian Ruiz.