Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi aanza na kipa wa Simba

GAMONDI Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo wa zamani wa Coastal Union, Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, Tanzania Prisons na KMC, amefunguliwa mlango wa kutokea Simba, jambo linaloipa ari Singida kuanza kumfuatilia ili kuinasa saini yake.

Singida Black Stars iliyopo chini ya Kocha Miguel Gamond, imedaiwa iko katika mazungumzo ya kuipata saini ya kipa wa Simba, Hussein Abel baada ya nyota huyo kumaliza mkataba alionao na kikosi hicho, huku kukiwa pia hakuna mazungumzo mapya ya kubakizwa msimu ujao.

Kipa huyo wa zamani wa Coastal Union, Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, Tanzania Prisons na KMC, amefunguliwa mlango wa kutokea Simba, jambo linaloipa ari Singida kuanza kumfuatilia ili kuinasa saini yake.

Taarifa zinaeleza, Abel anawindwa na Singida ili kwenda kuchukua nafasi ya Hussein Masalanga anayeelezwa huenda akaachana na timu hiyo msimu huu, baada ya kushindwa kupenya pia kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo, kimeliambia Mwanaspoti mbali na Masalanga ila mwingine anayeweza kutolewa ni Benedict Haule aliyeshindwa kupenya mbele ya makipa wenzao, Metacha Mnata na Mnigeria Amas Obasogie aliyesajiliwa Januari 2025.

“Abel ni chaguo sahihi kwetu na licha ya kutopata nafasi ya kucheza Simba mara kwa mara, ila tunaona anaweza kuleta sana ushindani mzuri kwa sababu hata huko alipotoka pia kila mmoja wetu aliuona uwezo aliokuwa nao,” kilisema chanzo chetu.

Kipa huyo aliyeanza soka la ushindani tangu 2014, akiichezea Madini FC ya jijini Arusha wakati ilipokuwa Ligi Daraja la Pili ambalo kwa sasa ni First League, ni miongoni mwa nyota wenye uwezo mkubwa jambo linaloivutia Singida kumhitaji.

Singida msimu ujao itayokuwa chini ya Kocha, Miguel Gamondi aliyerejea tena nchini baada ya kuifundisha Yanga kabla ya kuondoka Novemba 15, 2024, imepanga kufanya usajili mkubwa ili kuendelea kuleta ushindani katika michuano mbalimbali.

Timu hiyo iliyomaliza nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2024-2025 na pointi 57, itaiwakilisha nchi msimu ujao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiungana pia na Azam FC iliyomaliza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 63.