Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vázquez aibua upya kashfa ya Barcelona kuwahonga waamuzi La Liga

VAZQUEZ Pict

Muktasari:

  • Kashfa hiyo inahusiana na madai kuwa FC Barcelona ilifanya malipo kwa José María Enríquez Negreira, aliyekuwa makamu wa rais wa kamati ya waamuzi ya La Liga, kwa muda wa miaka kadhaa. Ingawa Barcelona imekanusha kuwanunua waamuzi, suala hilo limeendelea kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka.

Beki wa zamani wa Real Madrid, Lucas Vázquez amevunja ukimya kuhusu kashfa ya Negreira ambayo imelitingisha soka ya Hispania, akisema kuwa ni jambo gumu kuelezea na linaacha maswali mengi kuhusu uadilifu wa mchezo huo.

Kashfa hiyo inahusiana na madai kuwa FC Barcelona ilifanya malipo kwa José María Enríquez Negreira, aliyekuwa makamu wa rais wa kamati ya waamuzi ya La Liga, kwa muda wa miaka kadhaa. Ingawa Barcelona imekanusha kuwanunua waamuzi, suala hilo limeendelea kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka.

Akizungumza na vyombo vya habari, Vázquez amesema: “Ni vigumu kuelewa. Tunaambiwa malipo yalifanyika, lakini hakuna uthibitisho wa matokeo ya moja kwa moja uwanjani. Hata hivyo, kwa hadhi ya soka ya Hispania, hili ni jambo linalotia doa kubwa.”

Kauli hiyo inaongeza shinikizo kwa vyombo vinavyohusika kuendelea kuchunguza suala hilo kwa kina, huku mashabiki wakiendelea kusubiri ukweli kamili. 

VAZ 02

“Kuna mambo ambayo ni vigumu kuamini, na suala la waamuzi ni gumu sana, lakini kile kilichotokea kinastahili kujadiliwa,” amesema gwiji huyo wa Real Madrid.

“Kesi nzima ya Negreira ni ngumu kuielezea, ni ya kushangaza. Tulikuwa tunafahamu kila kitu, tulizungumzia hili ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo,” ameongeza.

Wakati huohuo, Lucas Vázquez amekiri kuwa video za Real Madrid TV zinazowalenga waamuzi mara kwa mara huongeza shinikizo kwa waamuzi wakati wa mechi.

VAZ 01


 
“Video za Real Madrid TV zinaweza kuwaathiri waamuzi kwa sababu nao ni binadamu, wana familia.”

Katika hatua nyingine mchezaji huyo amezungumzia mbio za ubingwa wa La Liga kati ya Barcelona na Real Madrid msimu huu na namna anavyoona hali inavyoendelea.

“Barça wana kikosi kizuri sana, ni burudani kuwatazama wakicheza. Itakuwa ligi ngumu sana, lakini natumai Real Madrid itashinda.”