Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UTAMU UPO HAPA: Newcastle inavyonogesha vita ya michuano ya Ulaya kwa kushinda Kombe la Ligi

UBINGWA Pict
UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Matokeo ya mechi hiyo ya Wembley yamekuwa na athari kubwa kwa namna ya timu zitakavyofuzu kwenye mikikimikiki ya michuano ya Ulaya, kwa sababu mshindi wa Kombe la Ligi, anapata tiketi ya kuanzia kwenye mchujo katika michuano ya UEFA Conference League.

NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United imeshinda taji lake la kwanza kwa msimu huu wa 2024/25 baada ya kuichapa Liverpool 2-1 kwenye fainali ya Kombe la Ligi iliyofanyika uwanjani Wembley, Jumapili.

Matokeo ya mechi hiyo ya Wembley yamekuwa na athari kubwa kwa namna ya timu zitakavyofuzu kwenye mikikimikiki ya michuano ya Ulaya, kwa sababu mshindi wa Kombe la Ligi, anapata tiketi ya kuanzia kwenye mchujo katika michuano ya UEFA Conference League.

Hata hivyo, kama Newcastle kwenye msimamo wa Ligi Kuu England itamaliza katika nafasi inayowapa tiketi ya kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao (kwenye Top Five), tiketi yao ya kuanzia kwenye mchujo wa Conference League itakwenda kwa timu inayofuatia kwa kushika nafasi ya juu kwenye msimamo, ambayo pia itakuwa haijafuzu moja kwa moja kucheza michuano hiyo ya Uefa kwa kupitia nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

UBI 01

Timu gani zitachuana kucheza Ulaya?

Tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya itazihusu timu nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Timu itakayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo, itapata pia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kuzingatia namna ambavyo klabu za Ligi Kuu England zitamaliza kwenye michuano ya Ulaya msimu huu na kuvuna pointi ambazo zitaifanya England kushika nafasi za juu kwenye chati za viwango vya Uefa. Kwa hali ilivyo, Ligi Kuu England ipo kwenye nafasi ya kuwa na timu tano zitakazochuana Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na kuna uwezekano timu hizo zikazidi na kufikia saba.

Kwa jinsi ilivyo, ili kufuzu UEFA Europa League kwa timu za England, zina nafasi mbili, moja ile ya kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi au timu inayoshika nafasi ya sita kama timu tano za juu zitakuwa zimefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na nyingine ni bingwa wa Kombe la FA, timu hiyo inafuzu kucheza Europa League.

Kwenye UEFA Conference League, washindi wa Kombe la Ligi wanaanzia kwenye mchujo wa michuano hiyo.

UBI 02

Mabadiliko yapo vipi?

Kama mshindi wa Kombe la FA atakuwa amefuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya au Europa League kwa kupitia tiketi ya nafasi yake kwenye msimamo wa Ligi Kuu England au kwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, nafasi yao kwenye Europa League itakwenda kwa timu inayofuatia kwenye nafasi katika msimamo wa ligi, ambayo itakuwa haijafuzu kwa michuano ya Uefa.

Na kama washindi wa Kombe la Ligi watakuwa wamefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya au Europa League kwa kupitia nafasi yao waliyoshika kwenye msimamo wa ligi au kwa kushinda moja ya michuano hiyo, basi tiketi yao ya kuanzia kwenye mchujo kwenye Conference League itakwenda kwenye timu inayofuatia katika msimamo wa Ligi Kuu England ambayo haijafuzu michuano ya Ulaya.

UBI 03

Newcastle imeshinda Kombe la Ligi, nini kitatokea?

Newcastle United imeshakamatia tiketi ya kucheza Conference League. Hata hivyo, bado ina matumaini ya kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya au Europa League msimu ujao kwa kupitia tiketi ya nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kama kikosi hicho cha kocha Eddie Howe kitatimiza lengo la kunyakua tiketi ya michuano ya Ulaya kwa kupitia nafasi yao kwenye msimamo wa ligi, basi tiketi yao ya Conference League itakwenda kwa timu inayofuatia kwenye nafasi ya msimamo wa ligi, ambayo itakuwa haijafuzu kucheza michuano ya Ulaya kwa kupitia nafasi yao katika ligi.

Jambo hilo linaweza kufanya hadi timu ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu kuwa na nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao. Kwanini inaweza kutokea timu 11 kufuzu kucheza Ulaya?

UBI 05

Huu ni mfano wa kile kinachoweza kwenda kutokea na kusababisha Ligi Kuu England kushuhudia timu itakayoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo huo kupata tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya (Conference League), endapo kama msimamo utabaki ulivyo hadi mwisho.

- Liverpool, Arsenal, Nottingham Forest, Manchester City hizo zitafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kumaliza Top Four.

- Newcastle itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kumaliza nafasi ya tano, ikiwa ni tiketi itakayotolewa na UEFA kutokana na kiwango cha timu za England kwenye michuano ya Ulaya msimu huu.

- Brighton itafuzu kucheza Europa League kwa kumaliza ligi kwenye nafasi ya sita.

- AFC Bournemouth itamaliza nafasi ya saba kwenye msimamo na kushinda tiketi ya Europa League endapo itashinda Kombe la FA.

- Chelsea itamaliza nafasi ya nane na kufuzu kucheza Europa League kwa kushinda ubingwa wa Conference League.

- Aston Villa itamaliza ya tisa na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kunyakua ubingwa wa taji hilo msimu huu.

UBI 04

- Manchester United au Tottenham Hotspur zitamaliza nafasi ya 10 na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kubeba Europa League.

Kwa kupitia mfano huo wa juu, tiketi ya Conference League iliyobebwa na Newcastle United kwa kushinda Kombe la Ligi haitakwenda kwa timu zilizopo kwenye 10 bora, kwa sababu zote zitakuwa zimefuzu michuano ya Ulaya, hivyo timu itakayokuwa kwenye Namba 11, ndiyo itakayokamatia tiketi hiyo na kwenda kucheza michuano ya Ulaya.

Hilo ndilo linaloweza kwenda kutokea endapo kama mfano huo utakwenda kutokea baada ya Newcastle kubeba Kombe la Ligi.