Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usishangae El Clasico ikipigwa Wembley

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Hispania imekuwa ikitumia Uwanja wa Olimpiki wa Catalonia kwa karibu miaka miwili wakati ikifanya maboresho ya uwanja wa Nou Camp.

MADRID, HISPANIA: KIPUTE cha El Clasico huenda kikahamishiwa Uwanja wa Wembley baada ya Barcelona kushindwa kukamilisha maboresho ya uwanja wao wa Nou Camp ambao utagharimu Pauni 1.25 bilioni.

Miamba hiyo ya Hispania imekuwa ikitumia Uwanja wa Olimpiki wa Catalonia kwa karibu miaka miwili wakati ikifanya maboresho ya uwanja wa Nou Camp.

Barcelona ina matumaini ya kurejea Nou Camp kabla ya msimu huu kufika mwisho na iliwekwa kwenye mpango wa kutumika katika mechi ambayo inatazamwa kama itaamua mbio za ubingwa wa La Liga dhidi ya mahasimu wao Real Madrid kwenye El Clasico, Mei 11.

Hata hivyo, mpango huo unaelekea kukwama baada ya kuripotiwa kwamba Nou Camp haionekani kama itakuwa tayari kabla ya msimu ujao haujaanza.

Uwanja huo ulivunjwa Juni 2023 na sasa ujenzi upo kwenye hatua ya msingi. Licha ya kupanga kutumia Pauni 1.25 bilioni kuboresha uwanja huo kutoka kuingiza watazamaji wanaoketi 99,354 hadi zaidi ya 105,000, mabosi wa Barca wana wasiwasi kama Nou Camp itakuwa imekamilika hadi kufikia El Clasico.

Hilo litawafanya mechi zao za mwezi wa mwisho wa msimu kutokuwa na uwanja wa nyumbani kwa sababu kibali chao cha muda cha kutumia uwanja wa Olimpiki kinakoma Aprili. Na sasa mpango wa kwanza ni kuongeza kibali hicho hadi kipindi cha majira ya kiangazi.

Lakini, uwanja huo wa Olimpiki wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 58,000 wameshachukuliwa kwa ajili ya matamasha mbalimbali kwa mwezi wa Mei, ikiwamo shoo ya Rolling Stones. Na sasa Barcelona inatazama uwezekano wa kuifanya mechi yao ya Real Madrid kwenda kucheza ng’ambo. Na kinachoripotiwa ni kwamba uwanja wa Wembley unatazamwa kama sehemu inayoweza kutumika, hasa kwa historia nzuri kwa Barcelona, ambapo walibeba Kombe la Ulaya la kwanza kwenye uwanja huo mwaka 1992. Uwanja huo wa Wembley una uwezo wa kuingiza watazamaji 90,000. Kwenye El Clasico mbili zilizopita, Barcelona iliichapa zote Real Madrid, mabao 4-0 uwanjani Bernabeu, Oktoba mwaka jana na 5-2 kwenye Spanish Super Cup huko Saudi Arabia.