Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usaliji wa Isak Liverpool wa aina yake

ISAK Pict

Muktasari:

  • Majogoo hao walimsajili straika huyo wa kimataifa wa Sweden,25, kwa dau kubwa la Pauni 130 milioni kutoka Newcastle baada ya sarakasi za muda mrefu juu ya dili hilo katika majira haya ya kiangazi.

LIVERPOOL, ENGLAND: IMEFICHUKA. Liverpool walilazimika kuwatumia wataalamu wao wa sayansi ya michezo kukamilisha usajili wa kihistoria wa dakika za mwisho wa Alexander Isak.

Majogoo hao walimsajili straika huyo wa kimataifa wa Sweden,25, kwa dau kubwa la Pauni 130 milioni kutoka Newcastle baada ya sarakasi za muda mrefu juu ya dili hilo katika majira haya ya kiangazi.

Isak aligoma kuichezea Newcastle baada ya Liverpool kukataliwa ofa yao ya awali lakini mazungumzo yaliendelea na baadae timu hizo zikakubaliana.

Hata hivyo, kulikuwa na kikwazo kikubwa ambacho Liverpool walipaswa kukishinda ili kukamilisha dili hilo.

Historia ya majeraha ya Isak iliwatia wasiwasi viongozi wa Liverpool wakati wa mazungumzo ya mkataba. Mshambuliaji huyo alikosa mechi 39 kati ya 114 akiwa Newcastle, tatizo kubwa likiwa jeraha la nyonga. Pia, alikosa zaidi ya siku 200 za mazoezi chini ya Kocha Eddie Howe.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sunday Mirror, Liverpool ililazimika kuwaomba wataalamu wao wa sayansi ya michezo kumfanyia vipimo vya kina ili kuhakikisha hali yake ya kiafya kabla ya kufikia makubaliano ya kumsajili.

Wataalamu wa masuala ya usajili walitaka kujiridhisha Isak hatokuwa mchezaji atakayekaa zaidi kwenye chumba cha matibabu.

Lakini wataalamu hao wa afya waliridhika kabisa na hali ya mwili wa Isak na wakaithibitishia Liverpool hakuna tatizo lolote, hivyo wanaweza kutumia rekodi ya ada ya usajili ya Uingereza kwake.

Pia, walisema wanaamini wanaweza kuboresha rekodi ya majeraha ya Isak ili kuhakikisha anakosa mechi chache kadiri inavyowezekana.

Imeelezwa pia atawekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kurejea kutoka majukumu ya kimataifa na Sweden.

Aidha, mpango maalum wa mazoezi tayari umeandaliwa ili kumsaidia kuongeza utimamu wa mwili kwa sababu alitumia muda mwingi wa majira ya kiangazi akijifanyia mazoezi peke yake.