Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili 2025/26, Arsenal ina jambo lake!

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Arsenal inamaliza msimu mwingine bila kubeba taji lolote msimu huu baada ya kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Paris Saint-Germain na mabosi wa klabu hiyo sasa wanatambua kwamba wanahitaji wanasoka wa viwango vya dunia kikosini.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake baada ya kuwa na mkwanja wa Pauni 150 milioni wa kutumia kwenye usajili wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huku mastaa saba wakitarajiwa kuonyeshwa mlango wa kutokea.

Arsenal inamaliza msimu mwingine bila kubeba taji lolote msimu huu baada ya kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Paris Saint-Germain na mabosi wa klabu hiyo sasa wanatambua kwamba wanahitaji wanasoka wa viwango vya dunia kikosini.

Na sasa klabu hiyo imepanga kuwa bize kwenye dirisha lijalo la usajili kunasa wakali wapya ili waje kuifanya Arsenal timu ya mataji msimu ujao.

Arsenal sasa haina shida kwenye kufungua pochi kunasa mastaa wa pesa nyingi, wakati ilipotumia zaidi ya Pauni 200 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi 2023 kunasa huduma za wakali Declan Rice (Pauni 105 milioni), Kai Havertz (Pauni 65 milioni) na Jurrien Timber (Pauni 35 milioni) – lakini, vipi kuhusu dirisha lijalo?

USAJ 01

Wanaosakwa

Mkurugenzi wa michezo mpya Andrea Berta kipaumbele chake kikubwa ni kunasa saini ya No9 mwenye uwezo wa kuifikisha Arsenal kwenye hatua za juu zaidi. Straika staa wa Newcastle United, Alexander Isak, 25, yupo kwenye chaguo la kwanza la kocha Arteta, akiamini huduma yake itakwenda kuwa na msaada mkubwa kwenye eneo ambalo ni dhaifu. Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden amefunga mabao 23 kwenye ligi msimu huu, lakini shida ni kwamba hataachwa kuondoka kwa rahisi na klabu yake baada ya kuipa ubingwa wa Kombe la Ligi na kwamba bei yake ni Pauni 150 milioni.

Ripoti zinafichua pia straika wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22, ambaye amewekwa kwenye mpango kwa sababu anapatikana kwa bei ndogo, Pauni 60 milioni. Wachezaji wengine kwenye orodha ya wanaosakwa na Arsenal ni pamoja na straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, 21 na fowadi wa Sporting CP, Viktor Gyokeres, 26, ambapo fowadi hao wawili wamefunga zaidi ya mabao 50. Staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams ni chaguo jingine kwenye safu ya ushambuliaji wanaosakwa na Arsenal, lakini tofauti na wachezaji wengine, saini yake inaweza kuwa ngumu kupatikana kutokana na mshahara mkubwa anaotaka.

Kuhusu kiungo itategemea na mazungumzo ya mkataba mpya wa Thomas Partey, lakini tayari kuna makubaliano ya kulipa Pauni 51 milioni huko Real Sociedad huko kumnasa Martin Zubimendi, 26, ambaye dili lake linaweza kukamilika wiki ijayo.

Kuna mipango pia ya kuwasaka staa wa Bournemouth, Dean Huijsen ambaye anatazamwa kama chaguo bora kwenye wingi sambamba na mkali wa Borussia Dortmund, Jamie Gittens ppamoja na kipa wa Espanyol, Joan Garcia wote wanahusishwa na Arsenal  na wapo kwenye msako wa kocha Arteta.

USAJ 02

Wanaoondoka

Ili kupata nafasi ya kuleta wapya kwenye kikosi, Arsenal italazimika kufungua milango ya wachezaji ambao inahisi haiwahitaji tena waendelee kuwamo kwenye kikosi chao. Oleksandr Zinchenko, Kieran Tierney na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wenye uwezekano mkubwa wa kuonyeshwa mlango wa kutokea, lakini majeraha ya goti ya Mbrazili huyo yamechelewesha ishu ya kupata ofa. Beki Nuno Tavares, viungo Fabio Viera na Albert Lokonga nao pia wanaweza kuondoka sambamba na Raheem Sterling, ambaye atarudishwa kwenye klabu yake ya Chelsea baada ya mkataba wake wa mkopo kufika tamati.

USAJ 03

Mikataba mipya

Taarifa nyema kwa mashabiki wa Arsenal ni kwamba klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kumsainisha mkataba mpya kipenzi cha kikosi hicho, Bukayo Saka.

Ripoti zinafichua kwamba mazungumzo yapo kwenye hatua nzuri na kwamba Saka atasaini mkataba mpya ambao utakwenda kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwenye Ligi Kuu England. Kuna mipango pia ya kuwapa mikataba mipya mastaa kama William Saliba na Gabriel – ambapo mabeki hao wa kati mikataba yao ya sasa itafika ukomo majira ya kiangazi 2027. Na wachezaji Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri, nao wataboreshewa mikataba ili kubaki kwenye timu hiyo na kucheza bila ya kushawishika na dili za kutoka nje.