Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastraika Isac, Ekitike wanavyosumbua vogogo

Muktasari:

  • Na kwenye swali hilo la nani anafaa, ndipo lilipoibuka hili la Hugo Ekitike na Alexander Isak.

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la usajili wa mastaa la majira ya kiangazi huko Ulaya lipo wazi na sasa gumzo kubwa ni kuhusu huduma za mastraika. Nani anafaa?

Na kwenye swali hilo la nani anafaa, ndipo lilipoibuka hili la Hugo Ekitike na Alexander Isak.

Ishu inaanzia kwenye bei, straika wa Eintracht Frankfurt, Ekitike si tu kwamba atapatikana kwa ada iliyopungufu kwa Pauni 50 milioni ukilinganisha na ile anayouzwa straika wa Newcastle United, Isak - bali pia anatazamwa kama bora ya wachezaji bora kabisa wa kuwa nao kwenye kikosi chao.

Na hilo ndio maana timu kama Liverpool na Arsenal zinaonekana kuwa siriazi kwenye mchakamchaka wa kumfukuzia straika huyo wa Ufaransa, hasa baada ya kile alichokifanya kwenye msimu wake wa kwanza kwenye Bundesliga, akisaidia Eintracht kukamatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Upande wa Isak, naye ni straika wa moto, lakini shida ipo kwa klabu yake ya Newcastle, inamuuza bei inayoanzia Pauni 150 milioni. Wakati Ekitike, Pauni 86 milioni tu inatosha.

Hata Newcastle United yenyewe ilikaribia kumsajili Ekitike kabla ya kumnunua Isak.

Lakini, kwa Liverpool na Arsenal usajili wa Isak unabaki kuwa ndoto yao kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi kwa sababu tayari ameshaonyesha ameweza kufanya kitu kwenye Ligi Kuu England, hivyo akitua kwenye moja ya timu hizo, ataendelea tu alipoishia.

Kingine, mabao ya Isak yalikuwa na mchango mkubwa kwa Newcastle kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Na ndilo linalowafanya Newcastle kumuuza straika huyo kwa bei mbaya, kwamba mnunuzi awe amedhamiria kwa dhati kunasa saini yake. Na umri wake ni miaka 25, anaweza kuuzika baadaye.

Newcastle inataka kumwongeza Isak mkataba wa miaka mitatu na kumwongezea mshahara kutoka huu anaolipwa kwa sasa wa Pauni 120,000 kwa wiki kama atasaini dili jipya.

Arsenal na hasa Liverpool ofa zao za mshahara zipo juu kuliko kiwango hicho. Kama Isak atagomea ofa ya Isak, basi Newcastle inaweza kushawishika kumpiga bei kwenye dirisha hili, hivyo Arsenal na Liverpool zinaendelea kusubiria msimamo wa Isak kabla ya dirisha hili halijafungwa.

Lakini, wakikwama huko haitakuwa kitu kibaya ikiamua kumchukua Ekitike kama mbadala wake na hakika huo utakuwa usajili bora zaidi kutokana na mavitu ya kibabe ya mkali huyo uwanjani.

Ekitike ana kimo cha futi 6 na inchi 3, ana ufundi miguuni na kasi kama Isak. Msimu wake wa kwanza Ujerumani baada ya uhamisho wa mkopo akitokea Paris Saint-Germain ulifanywa asajiliwe jumla, alifunga mabao 15 na asisti nane katika mechi 33 za Bundesliga.

Ni rekodi tamu kuliko straika anayewindwa na Arsenal, Benjamin Sesko, ambaye alifunga mabao 13 na asisti tano katika mechi 33, akiwa na kikosi cha RB Leipzig.

Ekitike na Omar Marmoush waliunda pacha matata sana Eintracht hadi hapo Marmoush alipohamia Manchester City kwenye dirisha la Januari. Hilo halikuwa na shida kwa Ekitike, ambaye alifunga karibu nusu ya mabao kwenye ligi akifunga mara sana na asisti tano baada ya Marmoush kuondoka.

Alikuwa tishio pia kwenye Europa League, ikiwamo bao lake la mbali alilowafunga Tottenham.

Ingawa Isak amefunga mabao mengi kuzidi Ekitike, lakini straika huyo Mfaransa ni hodari kwenye kuwatengenezea mabao wenzake na hicho ndicho kitu kinachompa nafasi kubwa ya kuwa chaguo bora.

Na uzuri, Eintracht ni klabu inayouza mastaa wake, ilifanya hivyo kwa Randal Kolo Muani, Marmoush na wengine kibao, hivyo haitaweka ngumu kwa Ekitike mkwanja mzuri ukiwekwa mezani.

Straika Ekitike anaripotiwa pia kuwa kwenye rada za Manchester United, ikimtazama kama mmoja wa mastraika inaowasaka kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.