Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Undani wa mlinzi wa Messi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hivi karibuni moja ya video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni ile iliyokuwa ikimuonyesha mwanaume mmoja aliyekuwa uwanjani wakati mechi inaendelea na kazi yake ikawa ni kumtazama Lionel Messi na kuhakikisha nyota huyo anakuwa salama muda wote, huyu ni Yassine Chueko.

Chueko, ambaye ameripotiwa kuajiriwa na mmiliki wa Inter Miami David Beckham amekuwa kitembelea kwenye eneo la pembeni ya uwanja kama usawa ambao Messi atakuwepo ili kuhakikisha hakuna mtu anayemvamia na kumsababishia madhara staa huyo wa kimataifa wa Argentina.

Mbali ya kumfata wakati anacheza uwanjani, pia mlinzi huyo huonekana akikimbia hadi eneo ambalo Messi atakuwa anashangilia baada ya kufunga bao.

Messi ambaye amejiunga na Inter Miami akitokea PSG akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika analindwa sana kutokana na wingi wa mashabiki wanaotamani kupiga naye picha, kumkumbatia na kukaa naye karibu kutokana na umaarufu wake.

Mlinzi huyu  ni mwanajeshi wa zamani wa jeshi la maji la Marekani ambaye kwa nyakati tofauti tofauti amewahi kuitumikia nchini hiyo kwenye misheni za kijeshi nchini Iraq na Afghanstan.

Mbali ya uzoefu ambao ameupata akiwa jeshini, Chueko pia ni mtalaamu wa mchezo wa masumbwi na Taekwondo na Mixed Martial Arts na kabla ya kuajiriwa kama mlinzi wa Messi alikuwa akifanya mazoezi na kufundisha watu baadhi ya michezo hiyo.

Vilevile licha ya kwamba yeye ndio amekuwa akionekana muda mwingi, uhalisia ni kwamba hafanyi kazi peke yake, kuna zaidi ya walinzi 50, ambao wote wana kazi ya kuhakikisha Messi anakuwa salama kabla na baada ya mechi kuisha na hata nyumbani kwake.

Kwa sasa, Chueko ndiyo anatajwa kuwa mlinzi mkuu wa staa huyu na amekuwa akimlinda pia kwenye mazoezi na sehemu za wazi ambazo Messi anatembelea.