Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martino: Tujifunze kushinda bila Messi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MIAMI, MAREKANI. KOCHA wa Inter Miami Tata Martino anasema wanatakiwa kujifunza kushinda mechi bila ya Lionel Messi baada ya nyota huyo kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Marekani maarufu MLS.

Messi alifunga bao hilo dakika ya 89 dhidi ya New York Red Bulls akitokea benchi Inter Miami ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo kwa mara ya kwanza kwenye ligi.
Messi alitazama bao la kuongoza la Inter Miami lilofungwa na Diego Gomez akiwa benchi kabla ya kuingia na kuweka kambani bao lake la 11 katika mechi tisa alizocheza tangu alipotua.
Martino aliamua kumpumzisha Messi mwenye umri wa miaka 36 kuelekea mchezo huo kwa sababu alicheza zaidi ya dakika 700 za mechi.

"Jambo muhimu ni kwamba tunathamini vijana wameshinda, lakini tunapaswa kuzoea na kushinda bila Messi," alisema Martino.

Leo atakosa michezo mitatu kwa sababu atakuwa katika majukumu ya mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia, Argentina itakuwa na mechi kuanzia Septemba, Oktoba na Novemba.