Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unamtaka Alaba? Wahi kajibebee fasta

ALABA Pict

Muktasari:

  • Alaba, 32, alijiunga na miamba hiyo ya Hispania kwa uhamisho wa bure Julai 2021 baada ya mkataba wake wa huko Bayern Munich ya Ujerumani kufika ukomo.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid imeripotiwa kujiandaa kumpiga bei beki matata kabisa, David Alaba kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Alaba, 32, alijiunga na miamba hiyo ya Hispania kwa uhamisho wa bure Julai 2021 baada ya mkataba wake wa huko Bayern Munich ya Ujerumani kufika ukomo.

Alaba ameitumikia Los Blancos kwenye mechi 116 katika michuano yote, akifunga mabao matano na kuasisti mara tisa, ikiwamo mechi 14 kwenye msimu huu wa 2024-25.

Staa huyo wa kimataifa wa Austria alikosa nusu ya kwanza ya msimu huu kutokana na kuwa na maumivu ya goti, alirejea uwanjani katikati ya Januari mwaka huu, lakini bado anapambana na hali yake kurudi kwenye kiwango bora.

Alaba hatacheza tena msimu huu baada ya kuumia kwenye goti la kushoto, lakini kuna uwezekano akarejea uwanjani wakati wa fainali za Fifa za Kombe la Dunia la Klabu litakapoanza katikati ya Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa Estadio Deportivo, Real Madrid inataka kumpiga bei beki huyo kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi na hilo ni kutokana na mshahara wake kuwa mkubwa, ambapo kwa sasa ndiye mchezaji anayeshika namba mbili kwa kulipwa mshahara mkubwa huko Bernabeu nyuma ya Kylian Mbappe.

Ripoti kutoka ndani ya Los Blancos inafichua kwamba wasiwasi mkubwa upo kwenye ufiti wa Alaba na mabosi wa klabu hiyo wanadhani huu ni wakati mwafaka wa kumpiga bei wakati mkataba wake ukitarajia kufika mwisho, Juni 2026.

Alaba amekuwa akisumbuliwa sana na maumivu ya goti, aliwahi kusumbuliwa Desemba 2023, ambayo yalikuwa na madhara makubwa kwenye maisha yake ya soka, ambapo alitumia muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja nje ya uwanja na kurejea mwanzoni mwa 2025. Alaba anaripotiwa kulipwa mshahara wa Pauni 370,000 kwa wiki Real Madrid, hivyo inaeleweka kwanini klabu hiyo inataka kuachana na mchezaji ambaye inadhani inamlipa mshahara mkubwa bila ya kupata inachokitaka kutoka kwake.

Kutokana na hilo, Alaba sasa kitu ambacho anaweza kukifanya ni kuhamia Saudi Pro League, mahali ambako anaweza kwenda kupata fursa ya kulipwa mshahara mkubwa kama ambavyo anaopokea huko Bernabeu.

Real Madrid inataka kuboresha safu yao ya mabeki kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, ambapo Lucas Vazquez naye anajiandaa kuondoka kwenye timu hiyo na kama Alaba ataondoka, kutakuwa na pengo kubwa kwenye safu hiyo.