Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unai Emery afunguka kitu Aston Villa

Muktasari:

  • Kocha huyo Mhispaniola alikasirika sana baada ya filimbi ya mwisho, huku Aston Villa ikikosa fursa ya kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Everton.

BIRMINGHAM, ENGLAND: KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery kwa hasira amesema timu yake haina nafasi ya kumaliza ndani ya tano bora baada ya Thierno Barry kuisababishia kipigo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo Mhispaniola alikasirika sana baada ya filimbi ya mwisho, huku Aston Villa ikikosa fursa ya kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Everton.

Mshambuliaji wa Everton alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga bao la dakika ya 59, huku kikosi cha David Moyes kilichojaa wachezaji wachanga kikiibuka na pointi zote ugenini Birmingham huko Villa Park.

Emery aliulizwa jinsi kipigo hicho kilivyoathiri nafasi za timu yake kusababisha presha kwa Arsenal na Manchester City, alisema: “Bado sisi si washindani wa kumaliza ndani ya tano bora. Tupo hapo kwa sasa, lakini hatujawa washindani wa kweli. Kuna timu nyingine zenye uwezo mkubwa kuliko sisi.”

Alipoulizwa kufafanua zaidi kauli hiyo, alikataa kujibu lakini alibainisha kuna wapinzani ambao wangependa kubadilishana nafasi na Aston Villa.

Emery aliwakumbusha mashabiki wake kuna timu nyingine ambazo zingefurahia kuwa kwenye nafasi walipo Aston Villa sasa.

Alisema: “Bila shaka tumepoteza nafasi nzuri sana. Lakini tuko mbele ya timu nyingine ambazo ni washindani wa kuwa kwenye nafasi tuliyonayo.

“Tulikuwa na nafasi ya kuwa wa pili kwenye ligi. Hilo lingekuwa jambo la kipekee sana. Lakini baada ya kuhisi maumivu ya matokeo haya, lazima tujaribu kurejea katika mwelekeo wetu mzuri wa kufanya mambo.”

Emery hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu jeraha la goti la nahodha, John McGinn ambaye alitolewa nje dakika ya 18. Baada ya jeraha hilo kwa mchezaji wa kimataifa wa Scotland, pamoja na kupotea kwa Boubacar Kamara wiki iliyopita na kutokuwepo kwa Donyell Malan, kocha huyo alisisitiza Aston Villa inapaswa kuingia sokoni kusajili wachezaji.

Alisema: “Tuna wachezaji wa kutosha kupata kiwango tunachohitaji. Lakini lazima tuwabadilishe baadhi ya wachezaji wanaoondoka.”

Kwa upande mwingine, kocha wa Everton, David Moyes alifurahi sana baada ya timu yake kupambana kwa nguvu na kupata ushindi wao wa tano ugenini msimu huu. Alikuwa na furaha zaidi kwa mfungaji wa bao la ushindi, Barry ingawa alimpongeza kwa tahadhari kwamba lazima aendelee kudumisha kiwango chake cha ufungaji, aliposema: “Ilionekana kama Thierno hakuwa na nafasi ya kufunga, lakini kuinua mpira juu na kuupitisha ilikuwa kazi ya hali ya juu sana.

“Ni vigumu sana kwa mchezaji yeyote kuja Ligi Kuu England na kuwa mshambuliaji wa kati ni kazi ngumu zaidi. Ukizingatia pesa nyingi zinazotumika kwa washambuliaji wengine, haimaanishi moja kwa moja mambo yataenda vizuri. Kama tulidhani angekuja na kufanya mambo makubwa mara moja kwenye Ligi Kuu, tulikosea. Lakini sasa tunahitaji nini? Yeye pamoja na Beto, nahitaji waniletee mabao.”