Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukata timu ya Ronaldo, mishahara ya wachezaji yacheleweshwa

UKATA Pict

Muktasari:

  • Klabu ya Al Nassr inakabiliwa na tatizo la kifedha ambalo limesababisha shughuli za usajili kusimama na malipo ya mishahara kucheleweshwa.

RIYADH, SAUDI ARABIA: UKIWA umebaki  mwaka mmoja wa mkataba wa Cristiano Ronaldo anaolipwa Pauni 488,000 kwa siku, klabu ya Al Nassr inakabiliwa na tatizo la kifedha ambalo limesababisha shughuli za usajili kusimama na malipo ya mishahara kucheleweshwa.

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimedai tatizo hilo limekuja siku chache baada ya kocha aliyeshinda Europa League, Ange Postecoglou, kuteuliwa kuinoa timu hiyo, na pia baada ya mgomo wa Ronaldo mapema mwaka huu kutokana na kile alichodai kutokuwepo kwa uwekezaji ndani ya klabu hiyo, licha ya yeye kulipwa pauni 488,000 kwa siku.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al-Riyadiyah, baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza walilipwa mishahara yao ya mwezi Juni kwa awamu, huku uongozi wa klabu ukiendelea kufanya juhudi za kulipa fedha zilizobaki unazodaiwa.

UKA 01

Hata hivyo, hakuna taarifa za kina kuhusu ni wachezaji wangapi wameathirika wala kiasi gani cha mishahara yao bado hakijalipwa na ni lini fedha hizo zitalipwa.

Kutokana na hali hiyo, ukubwa halisi wa matatizo ya muda mrefu ya kifedha ya klabu bado haujafahamika.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa madeni yaliyokusanyika  ambayo yanazidi mapato ya klabu  yamesababisha shughuli za usajili kusimama katika dirisha la sasa ukiwemo mpango wa kumsajili mchezaji wa kigeni wa kuchukua nafasi ya kiungo Marcelo Brozovic.

Hali hiyo tete inaweza pia kuwa na athari za muda mrefu kwa wachezaji waliopo ndani ya klabu, jambo lililosisitizwa na chanzo kilichonukuliwa na Al-Riyadiyah.

Ronaldo aligoma kucheza mapema mwaka huu kutokana na kile alichodai kutokuwepo kwa uwekezaji ndani ya klabu hiyo.

Habari hizi zinakuja siku chache baada ya Postecoglou, kuanza rasmi kazi ya kuinoa Al Nassr.

UKA 02

Chanzo hicho kilisema: "Hii inafanya isiwezekane kwa klabu kuingia katika majukumu mapya ya kimkataba kabla ya kushughulikia kwanza hali ya sasa ya kifedha na kutoa uthibitisho kwamba inaweza kutekeleza wajibu wake."

Chanzo hicho pia kilithibitisha kuwa uongozi wa Al Nassr bado haujawasilisha nyaraka zinazohitajika kwa mamlaka husika ili kuthibitisha uwezo wake wa kifedha wa kuingia mikataba mipya.

Yote haya yanatokea licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na klabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni tangu kuwasili kwa  Ronaldo, jambo lililoisaidia Al Nassr kurejesha ubingwa wa Saudi Pro League mwishoni mwa msimu uliopita baada ya miaka saba.

Mapema mwaka huu, Ronaldo  ambaye anaripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili majira ya kiangazi yaliyopita wenye thamani ya Pauni 492 milioni, alielezewa kutoridhishwa na kile alichokiona kuwa ni ukosefu wa uwekezaji katika kikosi.

Nahodha huyo wa Ureno pia anaripotiwa kutoridhishwa na namna Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) ulivyokuwa ukiiunga mkono klabu hiyo, hasa wakati wapinzani wake Al Hilal, ambao pia wanamilikiwa kwa asilimia 75 na PIF, waliendelea kuimarisha kikosi chao.

UKA 03

Miongoni mwa usajili mkubwa walioufanya ni wa aliyekuwa mchezaji mwenzake Ronaldo katika kikosi cha Real Madrid, Karim Benzema, ambaye alijiunga nao akitokea Al Ittihad.

Ronaldo alirejea uwanjani baada ya kukosa mechi mbili kufuatia kutimizwa kwa baadhi ya madai yake makubwa ambayo yalikuwa ni kulipwa mishahara iliyocheleweshwa pamoja na kurejeshwa kwa mamlaka ya uongozi wa klabu kwa watendaji wake wakuu.

Kutokana na hatua hiyo, Simao Coutinho (mkurugenzi wa michezo) na Jose Semedo (mtendaji mkuu), ambao walikuwa wamesimamishwa kazi na PIF, walirejeshewa  kuendelea na majukumu, kwa mujibu wa ripoti za wakati huo.

Ligi ilijibu kwa kusema: "Cristiano amekuwa akijihusisha kikamilifu na Al Nassr tangu alipowasili na amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo na malengo ya klabu. Kama mshindani wa kiwango cha juu, anataka kushinda. Lakini hakuna mtu mmoja, hata awe muhimu kiasi gani, anayefanya uamuzi unaozidi mipaka ya klabu yake."

Majira haya ya kiangazi, Al Nassr imemteua aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspur, Postecoglou, kuchukua nafasi ya Jorge Jesus.

Postecoglou amesema kupitia vyombo vya habari vya klabu mapema wiki hii: "Jesus alifanya kazi nzuri sana mwaka  uliopita kwa kushinda ubingwa na sasa klabu iko tayari kwenda hatua inayofuata, ndiyo maana nipo hapa."

Ameongeza: "Kila mwaka huwa ni mwanzo mpya. Nimepata mafanikio mengi katika kazi yangu, lakini kila msimu mpya naanza nikiwa na wazo lilelile kichwani  'nataka huu uwe mwaka bora zaidi kuwahi kutokea."