Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno akumbwa na matusi kisa Cristiano Ronaldo

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 alilazimika kufunga sehemu ya maoni kwenye chapisho lake la kwanza tangu Ureno itolewe, baada ya kukumbana na mashambulizi makali kutoka kwa mashabiki wa Ronaldo.

LISBON, URENO: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, amejikuta akipokea wimbi kubwa la matusi na lawama katika mitandao ya kijamii baada ya Ureno kutolewa kwenye Kombe la Dunia, huku baadhi ya mashabiki wakimlaumu kwa madai ya kumkwamisha Cristiano Ronaldo katika mashindano yake ya mwisho.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 alilazimika kufunga sehemu ya maoni kwenye chapisho lake la kwanza tangu Ureno itolewe, baada ya kukumbana na mashambulizi makali kutoka kwa mashabiki wa Ronaldo.

Katika ujumbe aliouchapisha Alhamisi, Fernandes aliandika:

“Nina huzuni, nimekata tamaa na nimevunjika moyo. Kikosi hiki kilinifanya niamini tunaweza kufanya makubwa, si kwa ubora wa wachezaji tu, bali pia kwa umoja tulioujenga kwa miaka mingi.”

Aliendelea: “Asanteni kwa wachezaji wote, benchi la ufundi na wafanyakazi wote waliokuwa nasi kila siku katika Kombe la Dunia. Pia nawashukuru sana Wareno wote kwa sapoti na imani yenu.”

BRUN 01

Alaumiwa kumhujumu Ronaldo

Baada ya sare ya mabao 1-1 dhidi ya DR Congo katika hatua ya makundi, Fernandes alikuwa mmoja wa wachezaji waliolengwa na mashabiki waliodai kuwa walimchezea vibaya Ronaldo kwa makusudi.

Mbali na Fernandes, Vitinha, Joao Neves na Pedro Neto pia walishambuliwa kwa madai ya “kumhujumu” nahodha huyo wa zamani wa Ureno.

Moto huo uliongezeka baada ya dada yake Ronaldo, Katia Aveiro, kupenda (like) chapisho la shabiki mmoja lililomkosoa Fernandes kwa kushindwa kuonyesha kiwango kizuri akiwa na timu ya taifa.

Chapisho hilo lilisema: “Ghafla walisahau jinsi ya kupiga pasi mbele, kunyang’anya mpira na kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza. Mchezo ukawa wa kurudisha mipira nyuma katikati ya uwanja. Kombe hili la Dunia limekuwa la ajabu sana.”

BRUN 02

Afunga maoni baada ya kushambuliwa

Baada ya kuchapisha ujumbe wake wa kuaga mashindano, Fernandes aliamua kufunga sehemu ya maoni kwenye akaunti zake kutokana na wimbi la mashambulizi.

Baadhi ya mashabiki waliandika: “Anajua kila mtu amegundua alikuwa akimchezea Ronaldo vibaya ili yeye aonekane zaidi.”

Mwingine amesema:”Kitendo cha Bruno kufunga maoni kinaonyesha kuwa yote yaliyokuwa yakisemwa kuhusu yeye na viungo wenzake ni kweli.”

Naye mwingine akaongeza:”Bruno ameonekana leo... lakini Instagram na X tu. Uwanjani hakufanya lolote, Ureno imetolewa halafu anafunga maoni.”

BRUN 03

Wapo waliomtetea

Hata hivyo, si kila shabiki aliyemlaumu Fernandes.

Mmoja wa waliomtetea aliandika: “Ronaldo si Messi. Ukiangalia mechi za Ureno utaona walijaribu kumpa mipira, lakini mara nyingi alikuwa amebanwa na mabeki.”

Aliendelea:”Tukubali ukweli kwamba akiwa na miaka 41 hana nguvu za kuanza kila mechi kama zamani. Bado anaweza kufunga mabao, lakini anahitaji nafasi na kasi ambazo sasa zimepungua. Acheni kulaumu wachezaji wasiokuwa na hatia.”

Brun 04

Ronaldo aaga Kombe la Dunia, Martinez pia asepa

Safari ya Ureno ilimalizika baada ya kufungwa bao 1-0 na Hispania katika hatua ya 16 Bora, bao la ushindi likifungwa na Mikel Merino dakika za mwisho.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa Cristiano Ronaldo katika historia ya Kombe la Dunia, baada ya kuthibitisha kuwa mashindano yaliyofanyika Marekani, Canada na Mexico ndiyo yalikuwa ya mwisho kwake.

Baada ya kutolewa, kocha Roberto Martinez naye alitangaza kuondoka kwenye nafasi yake.

“Nilikuja Ureno kwa lengo la kushinda Kombe la Dunia. Kwa kuwa sijafanikiwa, sioni sababu ya kuendelea. Mkataba wangu unaisha leo,” amesema Martinez.

Martinez anatarajiwa kurithiwa na Jorge Jesus, ambaye aliwahi kumfundisha Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr.