Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugumu wa kumng’oa Osimhen watajwa!

OSIMHEN Pict

Muktasari:

  • Hilo ni swali wanalojiuliza waliowengi, hasa ukizingatia Man United ilikuwa ikihitaji straika wa kiwango cha dunia kwenye dirisha hilo na Osimhen alikuwapo tu sokoni, anapatikana.

ISTANBUL,UTURUKI: KWANINI Manchester United haikumsajili Victor Osimhen kwenye dirisha lililopita?

Hilo ni swali wanalojiuliza waliowengi, hasa ukizingatia Man United ilikuwa ikihitaji straika wa kiwango cha dunia kwenye dirisha hilo na Osimhen alikuwapo tu sokoni, anapatikana.

Ukitazama namna anavyofunga mabao tena kwenye michuano mikubwa kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, tena akiwa kwenye timu kama Galatasaray, unaona kabisa angefaa kuwakimbiza mabeki wa timu pinzani kwenye Ligi Kuu England. Man United angewafaa.

Kwa mwaka huu wa 2025, straika huyo wa Kinigeria amezidiwa na Harry Kane (48) na Kylian Mbappe (47) pekee kwa idadi ya mabao waliyofunga kwenye michuano yote, ambapo hadi kufikia Novemba hii, mkali huyo ametupia nyavuni mabao 43.

Idadi hiyo ya mabao ni kubwa kuzidi mastraika wote wa Ligi Kuu England wanaoonekana kuwa ni mahodari wa kutikisa nyavu, ambapo Erling Haaland amefunga 30, Viktor Gyokeres amefunga 33 huku washambuliaji wengine kama Alexander Isak na Benjamin Sesko hata kwenye 10 bora ya waliofunga mara nyingi kwa mwaka huu hawamo.

Kwa kifupi tu, Osimhen amezaliwa kwa ajili ya kufunga, akikaa kwenye jungu moja na wapachikaji mahiri wa mipira nyavuni kama Haaland na Kane.

Straika huyo Mnigeria amefunga mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kuzidi wawili hao, Kane na Haaland baada ya kutupia hat-trick usiku wa Jumatano iliyopita na hivyo kumfanya awe amefikisha mabao sita katika mechi tatu alizochezea miamba hiyo ya Uturuki. Osimhen amefunga sita, wakati Kane, Haaland na Kylian Mbappe kila mmoja amefunga mabao matano kwenye mchakamchaka huo wa ufungaji bora Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kama Osimhen anafanya vizuri na kufunga mabao kwa namna anavyotaka kwenye michuano hiyo mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hawezi kushindwa kufanya hivyo kwenye Ligi Kuu England. Mikimbio yake ndani ya boksi umekuwa mtihani mkubwa kwa mabeki wa timu pinzani ni dhahiri angekuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha United ingenasa saini yake.

Kitu ambacho Osimhen anahitaji ni kupewa mipira tu anapokuwa ndani ya boksi, mengine atafanya mwenyewe. Kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi alionekana kuwa tayari kubadili timu baada ya kuonyesha kiwango bora kwa mkopo huko Galatasaray.

Jina la Osimhen lilitajwa sana sambamba na la Gyokeres kwamba ni mastraika wanaotazamiwa kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England.

Lakini, dirisha la usajili lilipofungwa, Gyokeres ndiye aliyefanikiwa kutua kwenye Ligi Kuu England akijiunga na Arsenal, ambako kwa sasa anakosolewa namna anavyoweza kushirikiana na wenzake, kitu ambacho inaaminika Osimhen asingekuwa na tatizo hilo.

Hata hivyo, sababu ya Man United kushindwa kumsajili Osimhen, ndiyo sababu hiyo hiyo iliyoifanya Chelsea kushindwa pia. Pesa. Osimhen, 26, bei yake aliyokuwa akiuzwa huko Napoli ilizifanya timu nyingi za England kujiweka kando. Kwa upande wa Chelsea, mshahara wa Osimhen ulikuwa upo nje ya viwango vyao hivyo ikawasajili Joao Pedro na Liam Delap.


Chelsea walidhani kwamba mmoja au wote wangeweza kufikia viwango vya kufunga kama Osimhen.

Man United nayo kwa muda mrefu imekuwa ikimsaka Osimhen na ilihitaji kumsajili Mnigeria huyo kabla ya kutua kwa Rasmus Hojlund. Kisha ilihamia kwa Benjamin Sesko kwenda kunasa saini yake kwa Pauni 74 milioni, huku ikimlipa mshahara mdogo kuliko anaolipwa Osimhen huko Galatasaray kwa sasa. Pesa ndicho kitu kilichowafanya Man United kwenda kumchukua Sesko na kumtengeneza kidogo kidogo kuliko kumchukua Osimhen, ambaye yupo tayari.

Man United ilifanya uwekezaji mkubwa kwenye safu yake ya ushambuliaji, ikimnasa Bryan Mbeumo kutoka Brentford na Matheus Cunha kutoka Wolves, ambao wanaungana na Sesko hakika kuhakikisha mabao yanapatikana. Lakini, hali ingekuwa tofauti kama ingefanikiwa kunasa saini ya Osimhen kutokana na uhodari wake wa kuweka mipira nyavuni.

Lakini, shida ipo kwenye pesa, kunasa huduma ya Osimhen kwa sasa, ada yake ni zaidi ya Pauni 100 milioni, huku mshahara wake utazidi Pauni 300,000 kwa wiki. Hicho ni kikwazo.