Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Osimhen aweka rekodi ya mabao Galatasaray ikiichapa Bodo/Glimt

Muktasari:

  • Katika ushindi wa mabao 3-1, mshambuliaji huyo wa Nigeria, ameonesha kiwango bora, akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kumsetia Yunus Akgun kufunga bao la tatu kipindi cha pili, na hivyo kuipa Galatasaray ushindi wa kwanza wa michezo miwili mfululizo kwenye michuano ya Ulaya tangu Desemba 2012.

ISTANBUL, UTURUKI: Victor Osimhen amefunga mabao mawili na kusaidia lingine wakati Galatasaray ikiendeleza mwenendo mzuri kwa kupata ushindi wa pili mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bodo/Glimt, mechi ikichezwa leo Oktoba 22, 2025 kwenye Uwanja wa RAMS Park, Uturuki.

Katika ushindi wa mabao 3-1, mshambuliaji huyo wa Nigeria, ameonesha kiwango bora, akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kumsetia Yunus Akgun kufunga bao la tatu kipindi cha pili, na hivyo kuipa Galatasaray ushindi wa kwanza wa michezo miwili mfululizo kwenye michuano ya Ulaya tangu Desemba 2012.

Mabao hayo mawili pia yamemfanya Osimhen kuwa mchezaji wa kwanza wa Galatasaray kufunga katika michezo saba mfululizo ya mashindano makubwa ya Ulaya, akivunja rekodi ya Burak Yilmaz aliyoiweka kati ya Oktoba 2012 na Machi 2013.

Andreas Helmersen aliifungia Bodo/Glimt bao la kufutia machozi mwishoni mwa mechi, timu hiyo ya mabingwa wa Norway ikiwa bado haijapata ushindi wowote katika hatua ya makundi.

Baada ya kuilaza Liverpool kwa taabu katika mechi iliyopita, ushindi huu umeipandisha Galatasaray chini ya kocha Okan Buruk hadi nafasi ya 11 kutoka ya 21 kabla ya mechi nyingine za leo Jumatano usiku kuchezwa.

Wenyeji walianza vizuri kwa kupata bao la mapema kupitia Osimhen, aliyepiga shuti la chini na kuutumbukiza mpira wavuni baada ya kupokea pasi ya Mario Lemina.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga bao lake la pili na la tano msimu huu dakika chache baada ya nusu saa, akitumia makosa ya nyuma ya Fredrik Bjorkan, kisha kumzunguka kipa Nikita Haikin na kutumbukiza mpira wavuni.

Osimhen angeweza kupata hat-trick yake ya pili ndani ya wiki moja baada ya kufanya hivyo kwa timu ya taifa ya Nigeria dhidi ya Benin Oktoba 14, 2025 lakini alipoteza nafasi mbili nzuri za kuongeza bao la tatu.

Hata hivyo, jitihada zake katika kumzuia beki Haitam Aleesami zilichangia bao la tatu, ambapo Yunus Akgun alipachika wavuni kwa jaribio la pili.

Kwa upande wa wageni, Jens Hauge alipiga nje akiwa katika nafasi nzuri, huku Sondre Fet akikosa kwa kugonga mwamba, lakini hatimaye walipata bao la kufutia machozi kupitia kichwa cha karibu cha Helmersen kufuatia krosi ya Bjorkan.

Bodo/Glimt sasa inabaki na pointi mbili kutokana na sare zao za awali na wako kwenye hatari ya kutolewa baada ya mechi tatu.