Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu za Afrika zaanza vibaya kombe la dunia U-17

Africa

MEXICO CITY, Mexico TIMU za Afrika zimeanza vibaya katika mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 17 baada ya Burkina Faso kukubali kufungwa bao 1-0 na Panama huku Ivory Coast ikifungwa mabao 2-1 na Australia. Baada ya mechi hiyo Australia itakutana na Brazil ambayo iliichapa Denmark mabao 3-0, wakati Ivory Coast itacheza na Denmark, huku Panama ikicheza dhidi ya Ecuador na Burkina Faso itacheza na Ujerumani. Katika mechi ya kundi E huko Queretaro kati ya Burkina Faso dhidi ya Panama, timu ya Panama iliweza kulisakama lango la Burkina Faso, ambapo katika dakika tatu za mwanzo mchezaji wa Panama, Alfredo Stephens alipiga shuti ambalo liligonga mwamba wa juu na baadaye kidogo Dario Wright aliunyanyua mpira juu na kumpita kipa wa Burkina Faso, Seni Ouedraogo, lakini mpira ulipita juu ya mwamba wa juu. Mpaka dakika 20 za mwanzo zinamalizika, Burkina Faso walikuwa hawajapiga shuti lililolenga goli, ambapo Panama wenyewe walikuwa wanatafuta kwa nguvu angalau kupata bao la kuongoza. Kufuatia makosa aliyofanya beki wa Burkina Faso, Issouf Paro baada ya kupiga kichwa mpira ambao ulimkuta Aguilar, ambaye alipiga shuti kali la mguu wa kushoto ambalo lilikwenda moja kwa moja nyavuni. Baada ya kufungwa bao hilo Burkina Faso walionekana kubadilika ambapo na wao walitengeneza nafasi nyingi za kushinda, lakini walishindwa kuzitumia na hadi wanakwenda mapumziko walikuwa wamepoteza nafasi kadhaa za kushinda kwa sababu Ben Zerbo na Ismael Bande walikuwa wakipiga mashuti yaliyokuwa yakitoka nje la lango. Katika mechi ya kundi F huko Guadalajara kati ya Australia na Ivory Coast, mchezaji Dylan Tombides wa West Ham United alionekana kukiongoza vema kikosi cha vijana wenzake, lakini tim u zote zilikuwa zikishambuliana. Walikuwa Ivory Coast ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 18 baada ya Drisse Diarrasouba kuwatoka mabeki wa Australia na kutoa pasi safi kwa Souleymane Coulibaly ambaye alipiga shuti lililokwenga moja kwa nyavuni. Katika kipindi cha pili, Australia walirudi kwa nguvu, ambapo katika dakika ya 51, Jess Makarounas aliisawazishia Australia bao, mchezaji huyo hakuwa akicheza vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini alipopata nafasi aliitumia ipasavyo. katika dakika ya 77, Australia ilipata bao la pili katika mchezo huo lililofungwa na Dylan Tombides baada ya mabeki wa Ivory Coast kujichanganya. Kocha wa Burkina Faso, Rui Pereira akizungumza baada ya mechi hiyo alisema,"kwa mtazamo wangu ilikuwa mechi nzuri ya soka, tulicheza vizuri, lakini katika kipindi cha kwanza tulizidiwa, katika kipindi cha pili tulishindwa kutumia nafasi tulizozipata, ila nakipongeza kikosi cha vijana wangu, pia bado zipo mechi mbili hatujacheza, kitu chochote kinawezekana, ninaamini ninacho kikosi kizuri, nitawaambia wachezaji wangu wajitume zaidi katika mechi ijayo." Kocha wa Ivory Coast alisema,"matokeo haya ni aibu kwetu, naamini tulistahili kushinda mechi hii, sisi tuliweza kumiliki mpira kwa asilimia 63, hata hivyo naweza kukiri kwamba wachezaji wangu walikuwa na wasiwasi kwa sababu ni mechi ya kwanza, lakini wachezaji wangu wana vipaji na pia ni wadogo, vile vile napenda kuwapongeza Australia kwa sababu wameshinda mechi."