Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tiketi ya UEFA kumpa Casemiro pesa ndefu

CASEMIRO Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa zamani wa Real Madrid kwenye mkataba wake huko Old Trafford kumewekwa kipengele kinachofichua kwamba mshahara wake utaongezeka kwa asilimia 25 endapo kama Man United itarejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Kibrazili, Casemiro anajiandaa kupokea nyongeza kubwa kwenye mshahara wake endapo kama Manchester United itanyakua ubingwa wa Europa League na kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Staa huyo wa zamani wa Real Madrid kwenye mkataba wake huko Old Trafford kumewekwa kipengele kinachofichua kwamba mshahara wake utaongezeka kwa asilimia 25 endapo kama Man United itarejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kama Man United itashinda mechi ya fainali ya Europa League itakayopigwa Bilbao, Mei 21, hiyo ina maana kutakuwa na nyongeza ya Pauni 100,000 kwa wiki kwenye mshahara wa Casemiro, jambo litakalomfanya awe analipwa Pauni 500,000 kwa wiki. Kiwango hicho cha pesa ndicho alichokuwa akilipwa Cristiano Ronaldo wakati alipokuwa kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Dili hilo lilikubalika wakati Casemiro alipotoka Santiago Bernabeu kwenda kujiunga na Man United mwaka 2022, wakati ambao timu hiyo ilikuwa haipo kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Jambo hilo linamweka njia panda kocha Ruben Amorim kwa sababu ongezeko hilo la mshahara linaweza kuwaibua mabosi wa timu hiyo ambayo kwa sasa wanabana matumizi, wanaweza kumfungulia mlango wa kutokea Casemiro, 33.

Mmiliki mwenza wa Man United, Sir Jim Ratcliffe alimwagiza kocha Amorim kupunguza mishahara kwenye kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu, wakati klabu hiyo kwa sasa ikipunguza wafanyakazi wengi ili kupunguza matumizi Old Trafford.

Wakati sasa Casemiro akiwa mchezaji anayelipwa zaidi Man United, yeye alikuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaweza kufunguliwa mlango wa kutokea ili kupunguza gharama.

Lakini, kocha Amorim bado anaona kuna kitu cha maana kutoka kwa Casemiro, ambaye kwa sasa amerudi kwenye kiwango chake bora. Alicheza kwa kiwango bora sana wakati Man United iliposhinda 3-0 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye nusu fainali ya kwanza ya Europa League. Man United ikiitupa nje Bilbao uwanjani Old Trafford, kikosi hicho kinachonolewa na Amorim kitakwenda kucheza na ama Tottenham Hotspur au Bodo-Glimt kwenye mchezo wa fainali utakaofanyika huko Bilbao, Hispania.