Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United ni wao tu kwa Osimhen, Chelsea yajitoa

TETESI Pict

Muktasari:

  • Ukiweka kando suala la straika Osimhen, Man United imeripotiwa pia kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Mbrazili, Matheus Cunha, ambaye amekubali kusaini mkataba wa kwenda kukipiga Old Trafford.

MANCHESTER United imeripotiwa kujiandaa kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kumpatia kocha Ruben Amorim kikosi ambacho kitakuwa na nguvu ya kushindana kwenye michuano yote.

Na katika hilo, kocha Amorim atahitaji pia kufungulia mlango wa kutokea mastaa kadhaa ili kupata nafasi ya kuleta wengine. Kwenye mchakamchaka wa kunasa mastaa wapya, Man United imeripotiwa kuwa kwenye wakati mzuri wa kunasa saini ya straika Victor Osimhen baada ya wapinzani wao kwenye mbio za kumfukuzia mshambuliaji huyo Chelsea kujiondoa kwenye mchakato.

Ukiweka kando suala la straika Osimhen, Man United imeripotiwa pia kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Mbrazili, Matheus Cunha, ambaye amekubali kusaini mkataba wa kwenda kukipiga Old Trafford.


Mason Greenwood

MASON Greenwood ameripotiwa kufungua milango ya kurejea kwenye Ligi Kuu England na jambo hilo limeanza kuziamsha klabu za nchi hiyo kufukuzia saini yake. Fowadi huyo aliachana na Manchester United kwa ada ya Pauni 26.6 milioni kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la mwaka jana kwenda kujiunga na Marseille kwa mkataba wa miaka mitano. Lakini, Machi mwaka huu, Greenwood alitibuana na kocha Roberto De Zerbi na sasa anafikiria kurudi EPL.


Viktor Gyokeres

ARSENAL inaripotiwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunasa huduma ya straika wa mabao Viktor Gyokeres katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kutengeneza kikosi kitakachokuwa na nguvu ya kushindana kwenye Ligi Kuu England. Arsenal inafahamu wazi eneo ambalo watahitaji kulifanyia maboresho makubwa katika dirisha lijalo ni kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati na hapo wanamtazama mkali wa Sporting Lisbon, Gyokeres kama mtu mwafaka.


Ademola Lookman

BARCELONA imeripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Atalanta BC, Ademola Lookman kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Staa huyo wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 27 amekuwa na kiwango bora sana kwenye kikosi cha Atalanta msimu huu, akicheza mechi 37 kwenye michuano yote, amefunga mabao 18 na kuasisti mara saba. Lookman amefunga mabao 13 na asisti 5 katika mechi 28.


William Saliba

REAL Madrid inaripotiwa kumweka beki wa kati William Saliba kwenye mpango wao wa wachezaji inaotamani kunasa huduma zao katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Saliba amekuwa na kiwango bora sana katika kikosi cha Arsenal msimu huu na jambo hilo ndilo linaloifanya Madrid kuhitaji akakipige kwenye kikosi chao kuanzia msimu ujao, ambapo kutakuwa na wachezaji kadhaa wa safu ya ulinzi watakaotemwa.


Antony

ARSENAL imeripotiwa kuwa na mpango wa kufanya uamuzi wa kushtukiza wa kunasa saini ya winga wa Manchester United, Antony, katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Antony amejipata tangu alipokwenda kujiunga kwa mkopo katika klabu ya Real Betis kwenye dirisha la Januari baada ya kucheza hovyo Man United alikojiunga kwa ada ya Pauni 85 milioni akitokea Ajax. Lakini, kiwango chake cha sasa kimevutia.


Samu Aghehowa

ASTON Villa imeripotiwa kukoleza mwendo kwenye msako wa straika wa FC Porto, Samu Aghehowa katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kwenda kukipiga huko Villa Park kuanzia msimu ujao. Hilo linakuja baada ya kuripotiwa kuna uwezekano mdogo kabisa wa Aston Villa kumchukua jumla Marcus Rashford.


Christopher Nkunku

MANCHESTER United imeripotiwa inaanza kufuatilia kwa karibu ripoti kwamba mshambuliaji wa Chelsea, Christopher Nkunku anajiandaa kuachana na Chelsea kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Mkataba wa sasa wa Nkunku utafika tamati 2029, lakini anataka kuondoka kwa sababu amekuwa hapewi nafasi.