Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Thomas Partey atoa ya moyoni

PARTEY Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa Atletico Madrid, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto, ni miongoni mwa wachezaji waliotangazwa na Arsenal kuwa wanaweza kuondoka bure.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Arsenal,  Thomas Partey amefunguka kuhusu hatima yake baada ya kuonekana katika orodha ya wachezaji waliotangazwa kuwa huru na Arsenal.

Kiungo huyo wa zamani wa Atletico Madrid, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto, ni miongoni mwa wachezaji waliotangazwa na Arsenal kuwa wanaweza kuondoka bure.

Hata hivyo, Arsenal bado inaendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumuongezea mkataba ili aendelee kubaki katika viunga hivyo vya Kaskazini mwa London.

Partey, ambaye kwa sasa yupo likizo, amezungumza na kituo cha 3Sports nchini Ghana, akibainisha kuwa furaha yake binafsi ndiyo kipaumbele chake, japokuwa wakala wake ndiye anasimamia uamuzi wote.

“Nadhani jambo la kwanza ni kujiuliza, wapi  unapojisikia furaha na kuona uko nyumbani?  Halafu unajiuliza lengo lako linalofuata ni nini, unataka kufanikisha nini. Lazima uzingatie hayo yote. Na mwisho wa yote, sote tuna familia inayohitaji pesa, hili ndilo tunalowaza.

“Hatuwezi kuwa na nguvu zile zile daima. Kuna mambo mengi ya kuzingatia ukiwa mchezaji mwenye familia, daima utahitaji familia yako iishi kwa furaha. Ukiwa mchezaji mwenye umri mdogo na huna familia, unaweza kucheza mahali popote, lakini kinyume cha hapo lazima utazame mambo mengi kabla ya kufanya uamuzi.”

“Mimi ni shabiki wa Arsenal, lakini siwezi kuamua lolote. Ninamuachia wakala wangu na timu. Mimi, nataka tu kufurahia soka.”

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amewahi kutoa maoni yake kuhusu Partey akisisitiza kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wake muhimu katika kikosi.

“Kwa upande wa Thomas, msimu huu amekuwa mzuri kwake. Namna alivyocheza na alivyokuwa akipatikana kila tulipomhitaji ilikuwa poa sana. Ni mchezaji muhimu sana kwetu.”

Partey alisajiliwa na Arsenal kutoka Atletico kwa pauni 45 milioni mwaka 2020 na tangu wakati huo ameichezea mechi 167 katika mashindano yote na kufunga mabao tisa.

Wakati Partey akitafakari hatima yake, Arsenal tayari imeanza kufanya mabadiliko kwenye safu ya kiungo kuelekea msimu ujao. Nyota wa zamani wa Chelsea, Jorginho, ameondoka na kujiunga na Flamengo ya Brazil.

Klabu hiyo pia inatarajiwa kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi, licha ya Real Madrid kuonyesha nia ya kuingilia dili hilo katika dakika za mwisho.