Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag kupewa mikoba ya Alonso

TEN Pict

Muktasari:

  • Ten Hag amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa Manchester United, Oktoba mwaka jana ameripotiwa kuwekwa kwenye mipango ya kupewa mikoba ya Alonso, ambaye anahusishwa na mpango wa kujiunga na Real Madrid.

MANCHESTER, ENGLAND: ERIK ten Hag amepiga hatua kubwa kwenye mazungumzo ya kurithi mikoba ya Xabi Alonso katika kikosi cha Bayer Leverkusen, imeripotiwa.

Ten Hag amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa Manchester United, Oktoba mwaka jana ameripotiwa kuwekwa kwenye mipango ya kupewa mikoba ya Alonso, ambaye anahusishwa na mpango wa kujiunga na Real Madrid.

Ripoti za kutoka Ujerumani zinafichua kwamba Ten Hag ameshajiweka tayari kwa ajili ya kwenda kuchukua mikoba ya Alonso, ambaye pia anajipanga kwenye kumrithi Carlo Ancelotti huko Real Madrid.

Ancelotti amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia kwenye soka la timu za taifa na amekuwa kwenye rada ya timu ya taifa ya Brazil kwa muda mrefu. Na Alonso kiwango chake bora Leverkusen kimemfanya aingie kwenye mipango ya Real Madrid - mahali ambako alitumika kwa miaka mitano alipokuwa mchezaji.

Alonso ambaye aliongoza Leverkusen kushinda ubingwa wa Bundesliga bila ya kupoteza mechi msimu uliopita, ataruhusiwa kuondoka kwa moyo mmoja na mabosi wa klabu hiyo ya Ujerumani, wanaoamini Ten Hag anaweza kuwa kocha wao mpya.

Leverkusen inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga msimu huu, ipo kwenye mazungumzo na Mdachi Ten Hag.

Ten Hag alifutwa kazi Man United, Oktoba mwaka jana licha ya kushinda Kombe la Ligi na Kombe la FA kwenye misimu yake miwili ya kwanza akiwa bosi wa kikosi hicho cha Old Trafford.