Arsenal yamkomalia Tchouameni dili la Saliba

Muktasari:
- Saliba ambaye anachukuliwa na kocha Mikel Arteta kama roho ya Arsenal katika ulinzi amekuwa mhimili kikosini tangu aliporejea kutoka Marseille na Nice alikodumu kwa misimu mitatu kwa mkopo. Real Mardid inamtaka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
ARSENAL imeiambia Real Madrid kuwa itakuwa tayari kumuuza beki wa kati wa kimataifa wa Ufaransa, William Saliba endapo tu itapewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo, Aurelien Tchouameni kama sehemu ya makubaliano.
Saliba ambaye anachukuliwa na kocha Mikel Arteta kama roho ya Arsenal katika ulinzi amekuwa mhimili kikosini tangu aliporejea kutoka Marseille na Nice alikodumu kwa misimu mitatu kwa mkopo. Real Mardid inamtaka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Kutokana na uchezaji wake, timu hiyo ambayo imekuwa ikiruhusu mabao yanayotokana na mipira mirefu imekuwa ikipambana kusaka beki atakayesaidiana na Antonio Rudiger kukabiliana nayo, ambapo chaguo la benchi la ufundi ni Saliba. Mchezaji huyo amecheza mechi 47 michuano yote msimu huu na kufunga mara mbili.
Calafiori
BBEKI wa kati wa Arsenal na Italia, Riccardo Calafiori, 33, anatakiwa na AC Milan ili kuimarisha safu ya ulinzi na tayari imeweka mezani Pauni 29.9milioni ili kumsajili wakati wa dirisha lijalo la majira ya joto. Tangu alipotua Arsenal, Calafiori amekuwa akipambana kuingia katika kikosi cha kwanza, ambapo inadaiwa kwamba ameomba pia kuondoka.
Daizen Maeda
MSHAMBULIAJI wa Celtic, Daizen Maeda anaweza kupatikana kwa takribani dau la Pauni 25 milioni ifikapo mwishoni mwa msimu huu, na kwa kiwango hicho tayari timu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham Hotspur ambazo zimekuwa zikimfuatilia zimeanza kupishana katika timu yake. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani.
Fermin Lopez
BARCELONA imekataa ombi ya Manchester United kwa ajili ya kumuuza kiungo Fermin Lopez katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Viongozi wa Man United walitumia ziara yao Hispania kuulizia juu ya kiungo huyo, lakini wakaambiwa watalazimika kulipa zaidi ya Pauni £42.7m ili kufanikisha dili hilo. Mkataba wake unamalizika Juni 30, 2029
Jamie Gittens
CHELSEA imepanga kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England, Jamie Gittens, 20, msimu ujao. Gittens ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Borussia Dortmund tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 12. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2028.
Tomas Soucek
KOCHA wa Everton, David Moyes, amewasilisha jina la kiungo wa West Ham United na timu ya taifa ya Jamhuri ya Czechechoslovakia, Tomas Soucek, 30, akitaka asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Soucek ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha West Ham United, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027 na amekuwa na ubora wa kipekee.
Lucas Paqueta
MABOSI wa West Ham United wanataka kiasi kisichopungua Pauni 70 milioni kwa ajili ya kumuuza kiungo wa kimataifa wa Brazil, Lucas Paqueta, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya kukusanya pesa kwa ajili kwa ajili ya kuboresha kikosi. Paqueta ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027, msimu huu amecheza mechi 33 na kufunga mabao matano.
Dario Essug
CHELSEA inatarajiwa kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon na Ureno, Dario Essugo katika dirisa lijalo la majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni 21 milioni baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu akiwa Las Palmas anayoichezea kwa mkopo. Mkataba wa Dario na Sporting Lisbon unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027.