Tambo zapamba moto kuelekea pambano la Pialali na Tinampay

Friday November 27 2020
DSTV PIC

Kuelekea pambano kali la kimataifa la ngumi kati ya Bondia mtanzania, Idd Pialali ‘Simba’ na Mfilipino Arnel Tinampay, tambo zimepamba moto, ambapo mabondia hao kila mmoja ametamba kuhakikisha anamkalisha mpinzani wake mapema tu kwenye pambano hilo litakalofanyika Novemba 28, 2020 kwenye ukumbi wa Next Door Arena jijini Dar es Salaam.

Pialali anataka kuwahakikishia Watanzania kuwa hapa hakuna ushindi wa pointi ni lazima mtu akae kwa KO mapema tu ili wasije wakazoea, hivyo amejiandaa kumchakaza mapema Mfilipino huyo.

Naye Tinampay akijibu tambo hizo alisema anatamani mashabiki wake waanze kutangulia pale Next-Door Arena kwa sababu kuna sapraizi ya burudani ya kutosha kwa ajili yao aliyoiandaa.

Tinampay amedai Pialali ni bondia mzuri lakini tayari amemsoma na haitakuwa ngumu kumpiga. Kama wewe ni mpenzi wa ndondi basi pambano hili sio la kukosa.

Kwa kuwajali wateja wake, DStv kupitia kifurushi cha Bomba cha shilingi elfu 19,900/= kwenye chaneli ya DStv 294 Plus itawaletea uhondo huo moja kwa moja kwenye sebule zao, Jumamosi kuanzia saa tatu kamili usiku. Lipia sasa kifurushi chako ili usipitwe na burudani hii ya kukata na shoka.

Advertisement