Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tajiri Man Utd... Tuna wachezaji wachovu tunawalipa pesa nyingi

TAJIRI Pict

Muktasari:

  • Man United imekuwa timu ya kiwango cha chini tofauti na ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson. Ndani ya miaka kadhaa tangu alipoondoka Ferguson, Man United ilifanya usajili wa mastaa kibao wenye majina makubwa na kuwasainisha mikataba ya pesa nyingi.

MANCHESTER, ENGLAND: BILIONEA mmiliki mwenza Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amekiri kwamba baadhi ya wachezaji hawana uwezo wa kutosha kuendelea kuwapo Old Trafford.

Man United imekuwa timu ya kiwango cha chini tofauti na ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson. Ndani ya miaka kadhaa tangu alipoondoka Ferguson, Man United ilifanya usajili wa mastaa kibao wenye majina makubwa na kuwasainisha mikataba ya pesa nyingi.

Baadhi ya sajili hizo za pesa nyingi zimekuwa janga la kiuchumi kwenye klabu, kitu ambacho bilionea Ratcliffe anajaribu kutaja wale waliopo kwenye timu na viwango vyao havifai.

Bosi huyo wa INEOS aliambia BBC: “Baadhi yao hawana uwezo na wanalipwa pesa nyingi. Kwa sasa tunahitaji kuwa na kikosi kinachowajibika na kinachopambana, inahitaji muda. Tupo kwenye kipindi cha mpito kuachana na yaliyopita na kufikiria yajayo.

“Kuna wachezaji wazuri kwenye kikosi, kama tunavyomfahamu nahodha wetu ni mchezaji makini. Bila shaka tunamhitaji Bruno Fernandes, ni mwanasoka bora sana.”

Ratcliffe anamiliki hisa asilimia 25 za klabu klabu hiyo alizonunua Februari 2024, ambapo alikubaliana na wamiliki wakuu, familia ya Glazer kwamba atasimamia masuala ya maendeleo ya soka. Na bosi huyo alishangazwa kuona malipo makubwa kwa wachezaji ambao viwango vyao vimekuwa vya kawaida.

Bilionea Ratcliffe alisema: “Kama ukiangalia wachezaji ambao tunanunua dirisha hili la majira ya kiangazi ambao bado hatujawanunua, tuliwanunua Antony. Tunamnunua Casemiro, tunamnunua (Andre) Onana, tunamnunua Hojlund, tunamnunua Sancho. Hivyo ni vitu tulivyovifanya huko nyuma, iwe tunapenda au hatupendi tumerithi hivyo vitu, lazima tumalizane navyo.

“(Jadon) Sancho anayechezea Chelsea kwa sasa tunalipa nusu ya mishahara yake, tutalipa Pauni 17 milioni hadi kufika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.”

Kocha Erik ten Hag alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo wakati Ratcliffe aliponunua hisa. Lakini, miamba hiyo ya Old Trafford ilimfuta kazi Ten Hag na kumpa kazi Ruben Amorim, Novemba, mwaka jana. Na tangu wakati huo, Man United imepoteza mechi tisa kati ya 26, huku ikiachwa nyuma kwa pointi 36 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu England, Liverpool.

Lakini, kocha huyo Mreno aliyewahi kuinoa Sporting Lisbon anaungwa mkono na Ratcliffe pamoja na mabosi wengine wakiamini ataiweka timu hiyo kwenye nyakati nzuri.

Ratcliffe alisema: “Nikikiangalia kikosi alichonacho Ruben nadhani anafanya kazi nzuri kwenye kusema ukweli. Nadhani Ruben ni kocha mahiri kijana. Ni kocha mahiri na nadhani atakuwa hapa kwa muda mrefu. Unaweza kuona kile anachofanya. Nadhani umeona alivyofanya dhidi ya Arsenal. Ni wachezaji gani dhidi ya Arsenal ambao walikuwa benchi ulikuwa unawafahamu? “Ni wangapi walikuwa wameshavaa jezi za Man United kikosi cha kwanza? Unaweza kuona hakuwa na kikosi. Ruben anafanya kazi kubwa sana.” Man United itashuka uwanjani Alhamisi mechi ya marudiano ya Europa League 16 bora dhidi ya Real Sociedad uwanjani Old Trafford.