Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sarr alipia bili ya umeme kijijini kwao Segenal

Muktasari:

  • Staa huyo wa Spurs ametumia mamilioni ya pauni kulipia huduma za umeme katika kijiji cha Fayako huko Senegal. Sarr alirejea kijijini Fayako, mahali ambako wazazi wake walitokea na kuwasaidia kulipia gharama za huduma ya umeme.

DAKAR, SENEGAL: KIUNGO staa wa Tottenham Hotspur, Pape Matar Sarr amelipa pesa kugharimia umeme wa kijiji kizima huko kwao Senegal.

Staa huyo wa Spurs ametumia mamilioni ya pauni kulipia huduma za umeme katika kijiji cha Fayako huko Senegal. Sarr alirejea kijijini Fayako, mahali ambako wazazi wake walitokea na kuwasaidia kulipia gharama za huduma ya umeme.

Alisema wakati alipotembelea Fayako, kisiwa kidogo kilichopo umbali wa maili 100 kutoka mji mkuu wa Senegal, Dakar: “Utaratibu unaendelea kuhusiana na huduma ya umeme. Nina hakika si muda mrefu, Fayako itapendeza kama watu wake wanavyopendeza. Nakipenda kijiji hiki na najivunia.”

Sambamba na kusaidia ulipia gharama za umeme, Sarr alichangia pia vifaa vya elimu kama laptop, printa na paneli za umeme wa jua katika shule za kijijini hapo.

Alitoa pia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya utanuzi wa kitua cha afya kwenye kijiji hicho. Sarr ameamua kufuata nyayo za shujaa wake, staa wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane, ambaye alichangia Pauni 500,000 kujenga hospitali kwenye mji wa kwao huko Bambali, Senegal.

Jamii yote ya Fayako, ikiwamo viongozi wa kijiji, walikusanyika pamoja kuonyesha heshima yao kubwa kwa staa huyo wa Spurs na kumbariki wakimwina mtoto wa kijiji.

Spurs ilifanikiwa kunasa kipaji matata kabisa wakati ilipomsajili Sarr wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akitokea Metz mwaka 2021, lakini alibaki kwenye timu hiyo kabla ya kutua rasmi huko London miaka miwili baadaye, ambapo mechi yake ya kwanza ilikuwa dhini ya Aston Villa, Januari 1, 2023. Tangu wakati huo amecheza mechi 81 kwenye ligi na kushinda ubingwa wa Europa League.